HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.
HOMA YA DENGUE
Homa ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu. Huweza kutokea katia maeneo ynye uoto wa kitropiki kama maeneo ya Afrika na Asia. Dengue kitaalamu pia hufahamika kama hdengue emorrhagic fever. Homa hii huweza kusababisha kushuka kwa presha ya damu, homa kali sana kutokwa na damu na hata kufariki.
Ugonjwa wa dengue huweza kuathiri mamilioni ya watu dunia nzima bado wataalamu wapo katika kutafuta chanjo ya ugonjwa huu. Kama ilivyo magonjwa mengine ya virusi dengue pia haina dawa maalumu, lakini mgonjwa atatibiwa kulingana na dalili anazoonyesha na hatimaye atapona. Wagonjwa wengi hupata nafuu dani ya wiki moja.
DALILI ZA UGONJWA WA HOMA YA DENGUE
1.homa kali sana inayofika nyizi 41 za sentigredi
2.Maumivu ya kicha
3.Maumivu ya misuli, viungio na mifupa
4.Maumivu nyuma ya macho
Pia unaweza ukaona dalili nyingine kama:-
1.kuenea kwa ukurutu mwilini
2.Kuchefuchefu na kutapika
3.Kutokwa na damu kwenye finzi na pua
ATHARI ZA KUCHELEWA KUTIBUWA KWA HOMA YA DENGUE
1.kutoka damu kwa wingi kwenye pua na mdomo
2.Maumivu makali sana ya tumbo
3.Kutapika kusikokoma
4.Kutokwa na damu chini ya ngozi
5.Matatizo kwenye ini, mapafu na moyo
6.Kifo
SABABU ZA HOMA YA DENGUE
Kama tulivyoona hapo juu kuwa homa ya dengue husababishwa na virusi ambao wanasambazwa na mbu. Pindi mbu kwenye virusi hawa akimng’ata mtu kumuachia virusi vya dengue.
NJIA ZA KUPAMBA NA NA HOMA YA DENGUE
Mpaka sasa hakuna chanjo ya homa ya dengue. Hivyo njia madhubuti na ya kipekee ni kujiepusha na kungwata na mbu aina ya Aedes aegypti. Kwa kutokomeza mazalia yote ya mbu karibu na maeneo unayoishi. Mbu hawa wanang’ata wakati wa mchana tofauti na mbu wanaoleta malaria ambao hung’ata wakati wa usiku.
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii itakwenda kuelezea mambo machache kuhusu ugonjwa wa kisukari
Soma Zaidi...Kabla ya kubanwa zaidi na pumu, kuna dalili za awali zinzznza kujitokeza, na hapo ndipo utakapoanza kuchukuwa tahadhari. Makala hii itakwenda kukujulisha zaidi kuhusu dalili hizo.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukujulisha dalili za kuwa huwenda una fangasi sehemu zako za siri.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ngozi kuwa kavu si mbaya, lakini inaweza kusumbua na isipendeze, ikitengeneza mistari laini na Mikunjo.
Soma Zaidi...Ni muda gani nitaanza kuona dalili za HIV na kilimo kitaonyesha kuwa nimeathirika?
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea ikiwa matibabu kwenye nyonga na kiuno hayatafanyika.
Soma Zaidi...Je na wewe ni katika ambao wanahitaji kujuwa dalili za mimba ndani ya wiki moja? kama ndio makala hii ni kwa ajili yako. Utakwenda kuona dalili za mwanzo sana za ujauzito toka siku za mwanzoni.
Soma Zaidi...ATHARI ZA KUTOKUTIBU MINYOO Kukaa na minyoo na kutoitibu kwa muda mrefu kunaweza kusababisha madhara mengi hususani kwenye ini na maeneo mengine ya mfumo wa kumeng’enya chakula.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na fangasi
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi upungufu wa damu unaosababishwa na minyoo dalili zake na namna ya kumsaidia mgonjwa mwenye tatizo hilo.
Soma Zaidi...