HOMA YA MANJANO (yellow fever)Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu.
HOMA YA MANJANO (yellow fever)
Homa ya manjano ni maradhi yanayosababishwa na virusi na husambazwa na mbu. Homa hii ipo sana nchi za Afrika na Amerika ya Kusini. Kwa hali ya kawaida homa ya manjano huweza kusababisha homa, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika. Pia homa ya manjano inaweza kuwa mbaya zaidi na kupelekea matatizo kwenye ini, figo na moyo pamoja na kutoka kwa damu yali inayotambulika kitaalamu kama hemorrhaging.
Inakadiriwa kuwa asilimia 50 ya wanaopata homa ya manjano wanafariki kwa maradhi maradhi haya. Tafiti zinaonyesha kuwa mpaka sasa hakuna tiba maalumu ya homa ya manjano, ila ipo chanjo kwa ajili ya kujikinga na virusi wanaosababisha homa hii.
Tafiti zinaonesha kuwa baada ya kungโatwa na mbu na kukuachia virusi hawa wa haoma ya manjano, virusi hivi huchukuwa siku tatu mpaka sita kumomaa. Kipindi hiki kitaalamu hufahamika kama incubation period. Katika kipindi hiki katu hutohisi dalili yeyote. Kisha hatua inayofuatainatambulika kama accute phrase kisha hatua ya meisho ni toxic phrase.
DALILI ZA HOMA YA MANJANO
A.Dalili za homa nya manjano katika hatua ya pili (Acute phrase)
1.Homa
2.Maumivu ya kichwa
3.Maumivu ya misuli hasa ya kwenye mgongo na magoti
4.Kutokufurahia mwanga wa jua
5.Vichefuchefu na kutapika
6.Kukosa hamu ya kula
7.Kuhisi kizunguzungu
8.Macho kuwa mekundu, uso na ulimu pia kuwa na rangi nyekundu
B. Dalili za homa ya manjano katika hatua ya pili (toxic phrase)
1.Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano
2.Maumivu yasiyo ya kawaida pamoja na kutapika damu
3.Kuongezeka kukojoakojoa
4.Kutoka na damu kwenye mdomo, pua na macho
5.Kupungua kwa mapigo ya moyo (bradycardia)
6.Ini na figo kushindwa kufanya kazi
7.Ubongo kushinwa kufanya kazi, vyema na kusababisha matatizo kama kifafa (seizure), kupoteza fahami (coma) pamoja na kuchanganyikiwa (delirium)
SABABU ZA HOMA NA MANJANO (YELLOW FEVER)
Kama tulivyokwisha kuona kuwa homa ya manjano husababishwa na virusi wanaoenezwa na mbua aina ya Aedes aegypti. Mbu hawa hukaa karibu na maeneo ambayo watu huwa wanaishi na huzaliana kwenye maji yaliyo safi. Virusi vya homa ya manjano vinaweza pia kuwaathiri manyani.
KUJIKINGA NA HOMA YA MANJANO
Ijapokuwa asilimia 20 mapa 50 ya wanaopata homa ya manjano hufariki, lakini itambulike kuwa mgonjwa anauwezo wa kupona kabisa endapo atawahi kupatiw matibabu. Zifuatazo ni baadhi ya njia tu za kujikinga na homa ya manjano
1.pata chanjo ya homa ya manjano
2.Jikinge na kungโatwa na mbu kwa:
?Kulala kwenye chandarua kizima na chenye dawa
?Kupaka losheni ya kuzuia mbu
?Kuondoa majimaji yaliyotuwama na kukata nyasi
Umeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za Kufunga kwa ulimi (Tongue-tie) kuanzia Mtoto anavyo zalia mpaka navyokua ni hali inayotokea wakati wa kuzaliwa ambayo kitaalamu hujulikana kama ankyloglossia.
Soma Zaidi...Minyoo ni katika parasite, yaani ni viumbe wanaokaa kwenye mwili na kujipatia chakula chake humo. Katika miili yetu minyoo huishi na kula kuzaliana na kukuwa. Kama unahitaji kujuwa wapi hasa wanakaa mwilini mwetu, endelea na makala hii
Soma Zaidi...Homa ni moka ya dalili inayohusiana na maradhi mengi sana. Unaweza kuwa na homa ikawa pia si maradhi kumbe ni stress tu. Je unasumbuliwa na homa za mara kwamara, Makala hii ni kwa ajili yako
Soma Zaidi...Tetekuwanga (varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, upele kama vile malengelenge. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya kawaida ya tetekuwanga, karibu watu
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza namna mbalimbali za kujikinga na VVU/UKIMWI
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dalili za mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.ni dalili ambazo ujitokeza kwa mtu Mwenye tatizo la mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu Cha mkojo.
Soma Zaidi...