Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.
Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kilo 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.
Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.
Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.
Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.
Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia mtoto akiwa na ugonjwa wa UTI.
Soma Zaidi...Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na uvimbe wa tishu za matiti kwa wavulana au wanaume, unaosababishwa na kutofautiana kwa homoni za estrojeni na testosterone. Pia unaweza kuathiri matiti moja au zote mbili, wakati mwingine bila usawa. Watoto wachanga,
Soma Zaidi...Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hukua kutoka kwenye tishu laini za misuli ya uterasi. Fibroids nyingi ambazo zimekuwepo wakati wa ujauzito hupungua au kutoweka baada ya ujauzito, kwani uterasi inarudi kwenye ukubwa wa kawaida.
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa Brucellosis ni maambukizi ya bakteria ambayo huenea kutoka kwa wanyama hadi kwa watu mara nyingi kupitia maziwa ambayo hayajasafishwa au kuchemshwa vizuri na bidhaa zingine za maziwa. Mara chache zaidi, ba
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za kujikinga na magonjwa, kwa kawaida tunajua wazi kuwa magonjwa yapo na yanasambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine na mengine hayasambai yanaweza kumpata mtu mmoja akapona au magonjwa mengine si ya kupona
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea namna na jinsi ya kujikinga au kuzuia Ugonjwa wa ini.
Soma Zaidi...