Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote
3.KISUKARI (DIABETES)
Mwili unahitaji nguvu na uwezo wa kufanya kazi, nguvu hii husababishwa na glucose iliyopo ndani ya mwili. glucose ni aina ya sukari ambayo hupatikana kwenye vyakula vya wanga. Mwili hauwezi kutumia glucose bila ya insulin. Insulin ni homoni ambayo inatengenezwa kwenye kongosho. Hii inakazi ya kudhibiti kiwango cha glucose ndani ya mwili. Yaani wakati kwenye damu kukiwa na glucose nyingi insulini huletwa ili kuipunguza na ikiwa ni kidogo insulin hailetwi.
Ikitokea mwili hauna uwezo wa kuzalisha insulini ya kutosheleza mwilini au seli zinashindwa kutumia insulini inayozalishwa hapa kisukari hutokea. Yaani mwili utashindwa kudhibiti kiwango cha glucose. Katika hali hii seli zitashindwa kupata glucose hivyo kusababisha damu kuwa na glucose nyingi na hivyo figo hutowa maji mengi na kusababisha kukojoa mara kwa mara. Katika hali hii tumesema kuwa glucose ni aina ya sukari ambayo inahitajika kwa ajili ya kupata nguvu na uwezo wa kufanya kazi (energy) hivyo mwili utatumia fat na protin kujitengenezea energy hivyo kupelekea kuzalisha sumu ndani ya mwli. Na hali hii ikiendelea mtu aanweza kupoteza fahamu na hali hii huitwa diabetic coma.
AINA ZA KISUKARI
1.Type 1 Diabetes; aina hii huotokea wakati mfumo wa kinga mwilini (immune system) unaposhambulia seli zinazozalisha insulin katika kingosho. Seli hizi zinaposhambuliwa mwili utashindwa kuzalisha insulin. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa aina hii ya kisukari husababishwa na virusi pamoja na kurithi kutoka kwa wazazi.
Aina hii ya kisukari pia huitwa insulin-dependent au juvenile diabees. Hii hutibiwa kwa kutumia dawa na mara nyingi huweza kuonekana kabla ya miaka 18. Dalili za aina hii ni za hatari sana na hutokea kwa ghafla. Miongoni mwazo ni kiu kikali, kuchoka sana na kupunguwa uzito.
2.Type 2 Diabetes; pia aina hii huitwa noninsulin-dependent diabetes na mara nyingi huwapata watu wenye umri wa kuanzia miaka 40 na wale watu ambao wana uzito wa kuzidi.
Katika aina hii ya kisukari mwili unazalisha insulin lakini seli zinashindwa kuitumia insulin inayozaliwa. Miongoni mwa dalili zake ni kukojoakojoa, kiu kikali, kutokuona kwa ufasaha, kuchelewa kupona kwa majeraha na maambukizi ya mara kwa mara.
3.Gestation Diabetes; hii huwatokea sana wajawazito mwishoni mwa mimba na hupotea baada ya mtoto kuzaliwa. Hii huweza kuongeza hatari wakati wa kijifungua na kama mama amerithi kisukari kutoka kwa wazazi hali inaweza kuwa mbaya zaid. Dalili zake ni sawa na zile za hizo aina mbili hapo juu,
KUPAMBANA NA KISUKARI
A)hakikisha una uzito wa kawaida
B)Wacha kutumia bidhaa za tumbaku
C)Punguza misongo ya mawazo
D)Fanya mazoezi ya mara kwa mara
E)Kula mlo kamili
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Posti hii inahusu dalili za figo.figo husawazisha maji mwilini pamoja na kuchuja mkojo.
Soma Zaidi...Makala hii itazungumzia dalili za Malaria, athari za kuchelewa kutibu malaria, na matibabu ya malaria
Soma Zaidi...Shinikizo la juu la damu ni hali ya kawaida ambapo nguvu ya muda mrefu ya damu dhidi ya kuta za ateri yako ni kubwa vya kutosha hivi kwamba inaweza kusababisha matatizo ya kiafya, kama vileรย Ugonjwa wa Moyo.
Soma Zaidi...Makala hii itakwenda kukupa elimu juu ya maradhi haya ya ukimwi, dalili zake, tiba na kinga zake na mengineyo zaidi.
Soma Zaidi...Kisukari cha Aina ya 2, ambacho wakati mmoja kilijulikana kama Kisukari cha watu wazima au kisichotegemea insulini, ni ugonjwa sugu unaoathiri jinsi mwili wako unavyobadilisha sukari (glucose), chanzo muhimu cha nishati ya mwili wako.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Dalili ambazo ujitokeza kwa mtu ambaye ana tatizo kwenye mishipa ya retina,ni tatizo ambalo uwakumba wafu wengi wenye matatizo ya kisukari.
Soma Zaidi...posti hii inazungumzia kuhusiana na Maambukizi kwenye mfumo wa mkojo ambapo kitaalamu hujulikana Kama UTI(Urinary Tract Infection (UTI)) hufafanuliwa kuwa ni maambukizo ya mfumo wa uzazi ambayo yanahusisha urethra.รย UTI ni maambukizi ya mfumo wa mkojo, m
Soma Zaidi...Ni ngumu kujuwa vidonda vya tumbo uhakika wake bila ya kupata vipimo. Unajuwa ni kwa nini, ni kwa sababu maumivu ya tumbo ni dalili ya shida nyingi za kiafya kama ujauzito, mimba, typhod, na shida kwenye unfumo wa chakula.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi ugonjwa wa tauni ambao kwa kitaalamu huitwa plague ni Ugonjwa unaosababishwa na wadudu ambao huitwa kitaalamu huitwa yersinia pestis ambao ukaa ndani ya panya.
Soma Zaidi...