image

nina maambukizi ya zinaha maumivu wakati wa kukojoa na usaha

Mimi nilifanya ngono isiyo salama Tar 14/07 mwaka huu, nilikutana tu na mwanamke ambae sikuwa hata na background yake yoyote hivyo baada ya siku tatu nilijikuta nina maambukizi ya zinaha (maumivu wakati wa kukojoa na usaha), hivyo nilienda hospital na kup

nina maambukizi ya zinaha maumivu wakati wa kukojoa na usaha

Mimi nilifanya ngono isiyo salama Tar 14/07 mwaka huu, nilikutana tu na mwanamke ambae sikuwa hata na background yake yoyote hivyo baada ya siku tatu nilijikuta nina maambukizi ya zinaha (maumivu wakati wa kukojoa na usaha), hivyo nilienda hospital na kupatiwa matibabu...



Namba ya swali 050

Baada ya kuanza dawa kwa muda kama wa wiki moja nilianza kupata maumivu ya kifua na kurudi hoapitali siku ya 12 baada ya tendo, nilipimwa vipimo vyote ikiwepo HIV na sikukutwa na chochote mpaka kufika siku ya 18 nikapata mafua ambayo yameambatana na homa kali na sijakutwa pia na malaria baada ya kwenda hospital, pia nina mamivu ya tumbo hasa sehemu ya chini na kitovu na kifua sehemu za manyonyo



Namba ya swali 050

Kwa muda huo wote toka pale nimekuwa natumia dawa tofauti za kifua, gesi tumboni, na mafua lakini mwili kwa sasa una maumivu makali mgongo, mikono na tumbo.



Namba ya swali 050

HIV haiwezi kuonekana kabla ya miezi mitatu



Namba ya swali 050

Dalili zake huanza kuja baada ya muda gani? Mheshimiwa pia kuhusu hizi changamoto zinaweza kuwa dalili za HIV? Leo ni siku ya 22 baada ya kitendo



Namba ya swali 050

Dalili zake zinanzia wiki ya kwanza mpaka miezi mitatu kisha zinapotea kabisa.



Namba ya swali 050

Dalili zake ni pamoja na mfua na homa Dokta?



Namba ya swali 050

Yes hizo ni dalili, ila zinawwza kuanbatana na mashambukizi mengi. Hivyo uhakika ni kupima baada ya miezi 3. Vipi ulipatabkuvimba mitoki, kwebye mapaja, shingo ama kwapa?



Namba ya swali 050

Hapana hiyo sijapata
mitoki ndio matezi?



Namba ya swali 050

Yes mitoki ni tezi



Namba ya swali 050

Zenyewe zinakuwaje, au ni uvimbe unatokea?



Namba ya swali 050

Hizi huwa ni katika viashiria vya mwanzoni sana, hata na huwapata watu wengi, sana



Namba ya swali 050

Hiyo sijawahi kupata kabisa, na mbaya zaidi nina hofu ambayo naona mpaka kufikia miezi mitatu itakuwa i,enipeleka pabaya zaidi, kwahiyo kwa kipindi cha miezi mitatu hii homa hazitakwisha?



Namba ya swali 050

HIV haipo hivyo kaka, yenyewe ipo siri sana. Inavijidaliki vichache sana, ambavyo sio rahisi kuviona kabisa. Homa kali, iloambatana na maumivu ya kifua, na mafua, huenda ni sababu nyingine kabisa. Ok, ulisema ulitokwa na usaha, bipo ulipopima walikueleza unanshida gani?



Namba ya swali 050

Walisema tu kwamba ni shida ya magonjwa ya zinaa ila sikuambiwa ni nini hasa hiyvo nilipatiwa dawa ambazo baada ya kutumia nimekuwa sawa kabisa na nilirudi kwaajili ya vipimo siku tatu baadae baada ya kumaliza dozi na sikukutwa na zile homa tena.



Namba ya swali 050

Yes huwenda ilokuwa ni kisonono.



Namba ya swali 050

Sawa dokta, naomba niwe naendelea kukujulisha hali yangu, lakini pia nipo Dar es Salaam kama naweza kuja kuonana kwa ushauri zaidi?



Namba ya swali 050

Ok



Namba ya swali 050





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 688


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Vyanzo vya minyoo
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyanzo vya minyoo Soma Zaidi...

Dalili za kifua kikuu (tuberculosis)
Kifua kikuu ni ugonjwa sugu wa kuambukiza na anuwai ya magonjwa ya kiafya yanayosababishwa na Mycobacterium tuberculosis complex. Kwa binadamu sababu ya kawaida ni Mycobacterium tuberculosis. Soma Zaidi...

Dalili za maambukizi kwenye uume
Post hii inahusu zaidi dalili za maambukizi kwenye uume, ni dalili ambazo ujitokeza pale maambukizi yanapotokea kwenye uume. Soma Zaidi...

Jinsi ya kujilinda na maradhi ya ini
Hapa nitakueleza namna ambavyounaweza kupunguza hatari ya kupata maradhi ya ini. Kwa njia hizi unaweza kujikina wewe na wengineo na maradhi haya hatari ya ini. Soma Zaidi...

IJUE HOMA YA CHIKUNGUNYA (CHIKV) DALILI ZAKE, TIBA YAKE, CHANJO YAKE, NA MBU ANAYESAMBAZA HOMA HII
Haya ni maradhi ambayo husambazwa kutoka kwa mtu kwenda kwa mtu kwa kupitia mbu. Soma Zaidi...

vidonda vya tumbo
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa mfumo wa kinga ya mwili inavyoshambulia ini.
Ugonjwa huu hupelekea kuvimba kwenye ini yako ambayo hutokea wakati mfumo wa kinga ya mwili wako unaposhambulia ini lako. Soma Zaidi...

Namna ya kufanya usafi wa sikio
Post hii inahusu zaidi namna ya kufanya usafi wa sikio, sikio ni mojawapo ya ogani ambayo usaidia kusikia,kwa hiyo sikio linapaswa kusafishwa kwa uangalifu kama tutakavyoona hapo chini. Soma Zaidi...

Ugonjwa wa kuharisha na sababu zake.
Kuharisha ni Hali ya kupitisha kinyesi Cha maji chenye damu au kisicho na damu Soma Zaidi...

Dalilili za maumivu ya kifua
Maumivu ya kifua huja kwa aina nyingi, kuanzia kuchomwa na kisu hadi kuuma kidogo. Baadhi ya Maumivu ya kifua yanafafanuliwa kama kuponda kuungua. Katika baadhi ya matukio, maumivu husafiri juu ya shingo, hadi kwenye taya. Soma Zaidi...

Dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa
Posti hii inahusu zaidi dalili za hatari kwa mtoto aliyezaliwa, ni dalili ambazo ujitokeza tu mtoto anapozaliwa kwa hiyo dalili hizi zinapaswa kuzuiwa ili zisilete madhara makubwa. Soma Zaidi...

MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
MWISHO Vidonda vya tumbo vinatibika bila ya shaka. Soma Zaidi...