Nina swali sheikh nahitaji msaada wa Elimu.
Nimeingia kwenye mgogoro na Mke wangu asubuhi hii kwa kuwa alikuwa akitamka maneno ambayo mimi sitaki kuyasikia kutoka kwake. Nimemuonya mara ya kwanza hakusikia, nikamuonya tena hakusikia, nikamuonya mara ya tatu kwa kumuambia kwamba *"Ukiniandikia tena Maneno haya basi nitakuwa nimekuacha"*. Naye akayaandika tena? Je, hapa talaka imetoka? Na hukmu yake ni ipi?