Zitambue aina zote za vyakule na ufanye maamuzi yaliyo kuwa sahihi katika uandaaji wa chakula chako
5.VYAKULA VYA VITAMINI
Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.
Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku.
Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa, na mboga za rangi nya njano.. vitamin hivi ni muhimu kwa kusaidia afya ya macho na mfumo wa upumuaji (respiratory track). Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea mtu kushindwa kuona wakati wa usiku. Mwili unakuwa ni rahisi kupata mashambulio pindi mtu akiwa na vitamin A kwa uchache.
Vitamin B1 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Husaidia katika kuhakikisha michakato ya kikemikali ndani ya seli inafanyika vizuri (metabolism). Pia husaidia katika kuunganisha taarifa za misuli. Ukosefu wa vitamin hivi unapelekea ugonjwa wa beriberi ambopo mtu anakosa hamu ya kula. Misuli kukaza pia ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi. Wakati mwingine moyo kushindwa kufanya kazi ni kutokana na upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin B2 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Husaidia katika ufanyikaji wa michakato ya kikemia ndani ya seli (metabolism). Kupasuka kwa midomo ni dalili ya ukosefu wa vitamin hivi
Vitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele usio kobolewa na hamira.. huhitajika kwa ajili ya kuwasaidia enzymes kubadilimchakula kuwa energy. Pellagra ni ugonjwa unaotokana na upungufu wa vitamin hivi. Mgonjwa anakosa hamu ya kula, misuli kukosa nguvu na kuharibika kwa ngozi.
Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa na maini. Husaidia katika utengezaji wa damu, na utengezaji wa genetic meterials. Ugonjwa wa anaemia, upungufu wa uzito na nerve damage hutokana na upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Husaidia mwili kufyonza madini ya chuma. Kukosa nguvu za misuli,na maumivu ya viungio(joints)kutokwa na damu kwenye mafinzi kuchelewa kupona kwa vidonda na kuumwa mara kwa mara ni dalili ya upungufu wa vitamin hivi.
Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini. Husaidia katika kukuwa na kuimarisha meno na mifupa. Ugonjwa wa matege kwa watoto na osteoporosis yaani mifupa kuwa milaini husababishwa na upungufu wa vitamin D.
Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na peanuts. Husaidi akatika kulinda utando uliopo ndani ya mwili. Mfumo wa fahamu kutokuwa katika hali ya kawaida ni dalili ya upungufu wa vitamin E
Vitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani. Husaidia katika kuganda kwa damu baada ya kupata jeraha. Damu kutoka kwa wingi baada ya jeraha ni upungufu wa vitamin K.
Mtu atapata matatizo pia kama hata kunywa maji ya kutosha kwa siku. Maumivu ya kishwa huweza kusababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Choo kuwa kigumu huweza kusababishwa na uchache wa kunywa maji.
6.MAJI
Zaidi ya 70% ya mwili wa binadamu ni maji. Tunahiyaji maji ili tuweze kuishi. Mmaji ni muhimu kwa afya. Mtu anahitaji kunywa maji bilauri 8 mpaka 10 za maji. Mtu anaweza kuishi siku ziaizopungua 8bila kunya maji lakini anaweza siku nyingi zaidi bila ya kutokula chakula.
Maji husaidia kurekebisha mifumo mbalimbali ndani ya mwili kama vile mfumo wa utoaji takamwili, mfumo wa chakula na mfumo wa damu. Maji husaidia katika kutibu maumivu ya kichwa amabayo yamesababishwa na unywaji mchache wa maji.
7.ROGHAGE(vyakula vyenye asili ya kambakamba)
Hii si katika aina vya virutubisho. Hivi ni vyakula ambavyo husaidia katika msukumo wa chakula tumboni. Husaidia katika kufanya haja kubwa itoke kwa usalama. Matatizo ya kuziba kwa choo au kupata hajakubwa kwa kiasi kidogo husababishwa na kutokula vyakula vyenye hali hii kwa kiwango kinacho hitajika.
Tunaweza kupata roughage kwenye nafaka zote zisizo kobolewa, matunda, maharage, kabichi spinach, mihogo na nyanya zisizo menywa na jamii zingine za vyakula hivi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1248
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Madrasa kiganjani
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake Soma Zaidi...
Faida za pilipili
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za pilipili Soma Zaidi...
VYANZO VYA VYAKULA VYA MADINI NA FAIDA ZAKE
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula Tikiti
Soma Zaidi...
Vyakula vyenye maji mengi kwa wingi
Soma Zaidi...
Faida za kula maini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini Soma Zaidi...
Vyakula vya vitamin D
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya vitamin D Soma Zaidi...
VINYWAJI SALAMA KWA MWENYE KISUKARI
Kuchaguwa vinywaji si jambo rahisi, lakini inabidi iwe hivyo kama una tatizo la kisukari. Je unasumbuka kujuwa vinywaji salama? makala hii ni kwa ajili yako, hapa tutaona vinywaji ambavyo ni salama kwa mwenye kisukari. Soma Zaidi...
Faida za kula stafeli/soursop
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za stafel/soursop Soma Zaidi...
Ni nini maana ya mlo kamili?
Mlo kamili ni mkusanyiko kuu wa vyakula mbalimba kwa pamoja huimarisha na kuujenga  mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.  Mkusanyiko wa vyakula vinavyotengeneza mlo kamili Kuna majina ya vyakula Soma Zaidi...
Faida za kiafya za Asali
Soma Zaidi...
Faida za kula tikiti
Somo hili linalenga kukujuza juu ya umuhimu wa tikiti kwenye afya ya mwili Soma Zaidi...