Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake
Vitamini E ni moja kati aya vitamini ambavyo vinapatikana kwenye vyakula, matunda na mboga. Pia unaweza kuvipata kwa njia ya vidonge kutoka kwenye maduka ya madawa. Kama vilivyo vitamini A, B, C, D na K vitamini E navyo endapo vitapungua mwilini kutakuwepo na madhara kiafya. Ijapokuwa upungufu wa vitamini hivi ni aghalabu sana kutokea. Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake.
YALIYOMO:
Maana ya Vitamini E
Mnamo mwaka 1922 wanasayansi wawili kwa majina ya Herbert Mclean Evans na mwenzie Katharine Scott Bishop waligundua vitamini E. baada ya ugunduzi wa vitamini E tafiti mbalimbali ziilifanywa katika kuonyesha ni zipi kazi za vitaini E mwilini. Kwa mfano Mwaka 1946 wanasayansi walikuwa wakifanya tafiti juu ya nadharia inayodai kuwa vtamini E husaidia dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu (coronary heart diseases). mwaka 1949 tafiti zilifanywa kuhusu nadharia ya kuwa vitamini E huweza kusaidia watoto njiti kuwakinga na maradhi kadhaa.
Kazi za vitamini E mwilini
Vitamini E katika miili yetu zina kazi kuu zifuatazo:
Vitamini E bi antioxidant, ndani ya miili yetu husaidia katika kuzuia athari za kemikali mbaya zifiharibu miiliyetu.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando wa seli,na kulinda seli dhidi ya uharibifu wa kemikali.
Husaidia katika ukuaji mzuri wa misuli.
Husaidia katika utengenezwaji wa utando maeneo mbalimbali ya mwili kama kwenye neva, mapafu, na maeneo mengine
Upungufu wa vitamini E
Upungufu wa vitamini E hutokea nadra sana lakini tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E vikipungua mwilini vinaweza kusababisha matatizo kwenye mfumo wa fahamu., ukuaji mzuri wa misuli na udhaifu wa misuli. Pia upungufu wa vitamini E unaweza kuathiri macho na hivyo kupelekea mtu kutoona vizuri.
Vyakula vya vitamini E
Tafiti mbalimbali kuhusu vitamini E
Tafiti hizi zilifanya lakini zinahitaji kuendelea zaidi maana bado majibu ya uhakika hayajapatikana juu ya matokeo ya tafiti hizo. Ijapokuwa maneno ni kama hivyo lakini ukweli ni kuwa vitamini E vina faida katika afya zetu:-
1. Mwaka 2017 tafiti zilifanya na kuonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kupunguza udhaifu wa misuli wakati wa kuzeheka
2. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E husaidia katika kulinda mtu dhidi ya maradhi ya ubongo kama kusahausahau na kuchanganyikiwa.
3. Tafiti zinaonyesha kuwa vitamini E mwilini husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya figo, kibofu, mapafu na korodani.
4. Husaidia kulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo na mishipa ya damu
5. Husaidia kwa wajawazito
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inaonyesha Faida za kula papai.papai Ni tunda na Lina leta afya,nguvu na kuujenga mwili.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula nyama
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...FAIDA ZA MATUNDA Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za matumizi ya vyakula vya asili, kama tunavyojua kwamba mababu na mabibi zetu walitumia vyakula vya asili wakaishi miaka mingi kweli.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula spinach
Soma Zaidi...Kuna aina nyingi za vyakula kama mafuta, wanga, fati, protini na vitamini. Je! unajuwa faida zake na hasara zake?
Soma Zaidi...