image

Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini

Fahamu vitamini B na kazi zake, Vyakula vya vitamini B na athari za upungufu wake

Vitamini B ni katika water soluble vitamin ambavyo vina kazi ya kuhakikisha kuwa michakato yote ya kikemikali mwilini inakwenda vizuri. Na hapa tunazungumzia kitaalamu metabolism. vitamini B vipo katika makundi mengi kma aB1, B2, B3, B5, B6, B7 na B12. katika makala hii nitakwenda kukueleza maana ya vitamini hivi, nini kazi zake hasa mwilini, wapi nitapata vitamini B na je ni zipi dalili za upungufu wa vitamini hivi.



Yaliyomo:

  1. Maana ya vitamini B
  2. Makundi ya vitamini B
  3. Kazi za vitamini B
  4. Vyakula vya vitamini B
  5. Upungufu wa vitamini B
  6. Athari za kuwa na vitamini B kupitiliza


Vitamini B ni nini?

Vitamini B ni katika kundi la vitamini vinavyofahamika kama water soluble vitamin. vitamini B ni kundi la vitamini ambavyo vinafanana sifa lakini vina utofauti kidogo. Vitamini B ndani ya miili yetu vinafanya kazi ya kuhakikisha kuwa michakato ya kikemikali inafanyika, michakato hiyo kitaalamu inafahamika kama metabolism.



Metabolism hii ni michakato ya kikemikali inayofanyika ndani ya seli kwa ajili ya mambo makuu matatu nayo ni:-

  1. Kubadili chakula kuwa nishati (nguvu)
  2. Kubadili chakula ama nishati kkuwa protein, carbohydrate, lipids na nucleic acid.
  3. Kuondoa uchafu na sumu mwilini (nitrogen waste)

Hivyobasi michakato hii yote ili ifanyike kwa ufasaha na ufanisi vitamini B vinahitajika katika miili yetu. Endelea kusoma makala hii ukaone kazi za vitamini B.



Makundi ya vitamini B

Makundi hayo ya vitamini B ni:

  1. B1 kitaalamu huitwa thiamine, hivi vimegunduliwa mwaka 1910 na mwanasayansi iliyeitwa Umetaro Suzuk Pia mwaka 1912 mwanasayansi aliyeitwa Casimir Funk aligundua thiamine.


  1. B2 kitaalamu huitwa riboflavinhivi navyo vimegunduliwa mwaka 1926 na wanasayansi wawili wanaokwenda kwa majina D.T Smith na E.G Hendrick.


  1. B3 pia hutambulika kama niacinau nicotinic acid kundi hili limegunduliwa mwaka 1937 na mwanasayansi anayekwenda kwa jina la Conrad Elvehjem.


  1. B5 na yo pia huitwa pantothenic acid, kundi hili limegunduliwa mwaka 1933 na Roger J. Williams


  1. B6 pia huitwa pyridoxine, pyridoxal, au pyridoxamine imegunduliwa na Paul Gyorgy mwaka 1934.


  1. B7 pia hufahamika kama biotinmwanasayansi aitwaye Margaret Averil Boas aliigundua vitamini hii miaka ya 1900


  1. B9 pia hujulikana kama folic acidMwanasayansi kwa jina la Lucy Wills aliigundua mwaka 1983


  1. B12 ama cobalaminshii imegunduliwa na jopo wanasayansi mbalimbali.


Kazi za vitamini B mwilini Na upungufu wa vitamini B mwilini

Kama tulivyoona kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-



B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.



B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.



B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo





B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.



B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.





B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.



Vyakula vya vitamini B

Tunaweza kupata vitamini B kwenye vyakula vifuatavyo:-

  1. Nyama
  2. Nafaka kama mchele, mtama, mahindi n.k
  3. Mimea jamii ya maharagwe kama kunde
  4. Viazi
  5. Ndizi
  6. Pilipili
  7. Mayai
  8. Mimea jamii ya karanga na alizeti
  9. Mboga za majani zenye kijani iliyowiviana na kutia weusi kama spinachi
  10. Matunda kama palachichi na ndizi


Dalili za upungufu wa vitamini B

  1. Kupata ugonjwa wa Anaemia huu ni upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
  2. Matatizo kwenye ngozi
  3. Kupata vidonda kwenye mdomo, ma kupasuka kwa mdomo
  4. Misongo ya mawazo ama kuchanganyikiwa
  5. Kuharisha
  6. Kupotesa kumbukumbu kwa urahisi
  7. Misuli kupoteza ujazo
  8. Kubadilika badilika kwa mood (fikra na hisia) yaani mara umekasirika mara umefurahi


Athari za kuwa na vitamini b kupitiliza

  1. Kichefuchefu
  2. Kuona maluelue
  3. Kutapika
  4. Kuharisha
  5. Maumivu ya tumbo
  6. Shida kwenye ngozi
  7. Kuzidi kwa kiu


Makala nyingine kwa ajili yako:

  1. Vyakula vya protini
  2. Vyakula vya vitamin K
  3. Vyakula vya vitamini C
  4. Afya ya uzazi
  5. Afya na magonjwa


                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 6573


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
2. Soma Zaidi...

Vyakula vya vitamin B
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamin B Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kunywa chai
Soma Zaidi...

Faida za kahawa mwilini.
Posti hii inahusu zaidi faida za kahawa mwilini, ni faida ambazo ujitokeza hasa kwa watumiaji wa kahawa. Soma Zaidi...

VYAKULA VYA PROTINI, FATI NA MAFUTA
Je! unatambuwa madhara ya vyakula vya protini na mafuta? ungana nasi kwenye somo hili Soma Zaidi...

Matunda yenye Vitamin C kwa wingi
Vitamin C ni katika vitamin vinavyosaidia sana mfumo wa Kinga kulinda mwili dhidi ya vimelea vya maradhi. Hapa nitakuletea orodha ya matunda ambayo yana vitamini C kwa wingi. Soma Zaidi...

Faida za kula Palachichi
Palachichi lina virutubisho vingi na vitamini, kula palachichi uiokoe afya yako Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kunazi/ lote tree
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kunazi/ lotetree Soma Zaidi...

Vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula hatari na salama kwa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Spinachi
Soma Zaidi...

Papai lililo iva ni salama kwa mama mjamzito au halifai
Papai ni moja kati ya matunda yenye vitamini C na virutubisho vinginevyo. Lakini papai pia ni moja kati ya vyakula ambavyo mjamzito anatakiwa awe makini navyo. Soma Zaidi...

Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume
Vijuwe vyakula vya kyongeza nguvu za kiume na mambo yanayopunguza nguvu za kiume Soma Zaidi...