2.
2.UPUNGUFU WA VYAKULA HIVI NA MADHARA YAKE.
Kama tulivyosema huko awali kuwa upungufu wa chochote katika vyakula hivi unaweza kuleta madhara zaidi. Halikadhalika kuzidi kwa baadhi ya virutubisho mwilini kunaweza kusababisha madhara. Kwa mfano madini ya chumvi yakizidi zaidi mwilini yanaweza kusababisha presha ya kushuka. Halikadhalika madini ya chuma yakizidi pia ni hatari.
Mwili unahitaji virutubisho hivi kwa kiwango maalumu. Na mwili wenyewe unafanya kazi hii ya kuchukua kiwango unachohitaji na kinachozidi kinatoka kwa njia ya haja kubwa au ndogo. Sasa hebu tuone kwa ufupi vyakula hivi vinaleta adhari gani pindi virutubisho vikipungua.
v
1.UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
1.Madini ya sodium (table salt) Upungufu wa madini haya utapelekea udhaifu wa misuli na udhaifu wa mifupa. Pia mapigo ya moyo kutokuenda vizuri husababishwa na upungufu wa madini haya.
2.Madini ya chuma. Upungufu wa madini haya hupelekea matatizo katika mfumo wa damu. Ugonjwa wa anaemia unamahusiano ya moja kwa moja na upungufu wa madini ya chuma. Madini ya zink, hupatikana kwenye kamba, kaa, nyama na hamira. Husaidia pia katika afya njemaya mfumo wa kinga (immune system) na uponaji wa majeraha.
3.Madini ya kashiam(calcium). Madini haya yakipunguwa mwilini mifupa na meno huwa na udhaifu. Halikadhalika damu hutoka kwa muda mrefu baada ya jeraha kabla ya kuganda.
4.Madini ya phosphorus,Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.
5.Madini ya Potashiam (potassium) husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini. Upungufu wa madini haya unaweza kupelekea matatizo katika misuli.
6.Madini yakopa ( copper) Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea urahisi katika kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo mkatika mifupa na viungio (joints).
7.Madini ya manganese Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea kupoteza kwa joto mwilini, mifupa kuwa nyepesi, kutokwa na damu za pua na kupata kizunguzungu.
8.Madini ya iodine Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid. Ugonjwa wa goita (goiter) husababishwa na upungufu wa madini haya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika post hii utakwenda kujifunza aina 20 za vitamini. Utajifunza kazu zake mwilini, vyanzo vyake na madhara yanayoweza kutokea kutokana na upungufu wake.
Soma Zaidi...FAIDA ZA MATUNDA Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi kazi ya majani ya mstafeli dhidi ya bakteria na fangasi, pamoja na kutibu saratani mbalimbali na upambana na fangasi na bakteria kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya vitamini na faida zake
Soma Zaidi...unayopaswa kuyajuwa kuhusu protini na vyakula vya protini, faida zake na hasara zake. Madhara ya kiafya yanayohusiana na protini pamoja na kuyaepuka madhara hayo
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha vyakula ambavyo ni vizuri kwa mwanamke anayenyonyesha ili kumsaidia kupata maziwa kwa wingi.
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kukufundisha faida za kiafya za kula asali
Soma Zaidi...Hapa utajifunza vyakula hatari kwa mgonjwa wa kisukari, pia utajifunza vyakula salama anavyotakiwa ale mgonjwa wa kisukari, Pia ujajifunza njia za kujikinga na kisukari
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula peazi/peas
Soma Zaidi...