MAUMIVU YA UUME BAADA YA TENDO LA NDOA




Kushiriki tendo la ndoa ni jambo linalopelekea furaha na afya pia ya kimawazo na kijamii. Lakini furaha hii wakati mwingine hufuatiliwa na majuto ma maumivu makali ya uume baada ya kumaliza tendo la ndia. Maumivu haya pia yanaweza kutokea wakati wa tendo la ndo. Maumivu haya ya uume ni vigumu kuyaelezeaa, ila tambuwa tu kuwa uume unapatwa na maumivu. Maumivu haya wakati mwingine yanapelekea kuhisi kama unaunguwa kwenye uume.



Sababu za maumivu:
1.Ugonjwa wa UTI
2.Tezi dume
3.Kushambuliwa kwa mirija ya mkojo na bakteria
4.Kuwa na fangasi kwenye uume
5.Kama hujatahiriwa
6.Maradhi ya ngono kama gonoria
7.Uke kuwa mkavu
8.Mkao uliotumika katika tendo amoja na namna ya tendo lilivyofanyika
9.Kuwa na aleji
10.Kuathirika kwa tishu za uume
11.Kupinda kwa uume.
12.Kama tendo limefanyika kwa muda mrefu
13.Kama uume ni mnene sana



Nini matibabu ya tatizo:
1.Hakikisha uke una majimaji ya kutosha
2.Tumia vilainishi
3.Fanya tendo kipolepole
4.Tumia mikao rafiki na isiyo na tabu
5.Tibu magonjwa kama gonoria, UTI na tezi dume
6.Tibu fangasi
7.Kama unafanya tendo la ndoa kwa zaidi ya dakika 30, jitahidi upunguze ama uwe unapumzika.