Sababu za uvimbe kwenye matiti na dalili zake kiafya.
TATIZO LA UVIMBE KWENYE MATITI (MAZIWA)
Katika hali ya kawaida vimbe nyingi kwenye matiti hazina athari kubwa za kiafya na huondoka zenyewe. Hata hivyo zipo ambazo zinachelewa kuondoka ama haziondoki kabisa. Vimbe hiz huweza kusababishwa na mabo mengi. Lakini zipo chache husababishwa na saratani. Vimbe kwenye matiti mara nyingi si zenye kusababisha maumivu ama kutokwa na majimaji ama maziwa ama damu kwenye chuchu. Je unasumbuliwa na uvimbe wa kwenye matiti, makala hii ni kwa ajili yako.
Sababu za uvimbe kwenye matiti
1.Matiti kujaa majimaji kwenye vijishimo vidigovidogo vilivyomo ndani ya titi
2.Vijitundu vidogovidogo ndani ya titi kujaa maziwa (hutokea wakati wa kunyonyesha)
3.Tishu za kwenye ziwa kuwa kama linyama
4.Majeraha
5.Kuwa na infection (mashambulizi ya bakteria) kwenye titi
6.Saratani ya ziwa
7.Kuota kwa vijinyama kama chunjuwa kwenye mrija wa maziwa
Muda wa kumuona Daktari
Kama ulivyosoma hapo juu kuwa uvimbe wa titi unaweza kuondoka wenyewe bila hata ya kuhitaji dawa. Lakini hutokea ikahitaji kumuona daktari endapo:-
1.Umeingezeka mwingine
2.Uvimbe haukuondoka hata baada ya kupata hedhi
3.Uvimbe unazidi kuwa mkubwa
4.Ziwa limeanza kuonyesha michubuko
5.Ngozi ya ziwa kubadilika rangi
6.Maumbile ya chuchu kubadilika
7.Chuchu kuanza kutoa damu
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Kitabu cha Afya 👉2 Bongolite - Game zone - Play free game 👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 ai web app 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Yajue mazoezi ya kegel
Posti inahusu zaidi mazoezi ya kegel, ni mazoezi ambayo ufanywa na watu wengi na sehemu yoyote yanaweza kufanywa kama vile chumbani, sebuleni, uwanjani na sehemu yoyote ile na kwa watu tofauti.
Soma Zaidi...Jinsi ya kushusha homoni za kiume.
Posti hii inahusu zaidi njia ambazo unaweza kuzitumia ili kuweza kupunguza homoni za kiume kwa akina dada.
Soma Zaidi...Mwanaune anapataje fangasi kwenye uume
Post hii itakujulishs kwa namna gani mwanaune anaweza kupata fangasi kwenye uume wake
Soma Zaidi...Kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa.
Post hii inahusu zaidi kuvunjika kwa mtoto wakati wa kuzaliwa, hali hii utokea kwa watoto wadogo wakati wa kuzaliwa kwa sababu maalum kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Kazi za homoni katika Mzunguko hedhi.
Post hii inahusu zaidi kazi za homoni katika Mzunguko wa hedhi, katika kipindi hiki kuna homoni mbalimbali ambazo ufanya kazi kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Namna ya kutunza uke
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza uke, tunajua wazi kuna magonjwa mbalimbali yanayoweza kutokea iwapo uke hautaweza kutunzwa vizuri na pia uke ukitunzwa vizuri kuna faida ya kuepuka maradhi ya wanawake kwa njia ya kutunza uke.
Soma Zaidi...