Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Yanayochochea zinaa ni pamoja na mavazi yasiyozingatia sheria ya Kiislamu; michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia sheria ya Kiislamu; michezo, miziki, ngoma, nyimbo na mengineyo yanayochochea zinaa.
"… Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)" (17:32)
Uchafu na ubaya wa zinaa unadhihirika wazi kwa wahusika binafsi na kwa jamii kwa ujumla katika maeneo yafuatayo:
(i)Magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI, ambayo hudhoofisha afya na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
(ii)Kuporomosha maadili ya jamii. Watu wazinifu hawana haya, ni watovu wa nidhamu, walaghai, waongo, wabinafsi na wapupia machafu ya kila namna.
(iii)Zinaa huondosha umuhimu na heshima ya ndoa.
(iv)Kuvunja ndoa na kusababisha matatizo ya kifamilia.
(v)Husababisha watoto wa mitaani na kuingiza jamii katika janga la wahuni, wala unga, matapeli, majambazi pamoja na kusababisha kundi kubwa la vijana wasio na uwezo wa kufanya lolote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Malaika wamepewa kazi ya kumtumikia Allah(SW) kwa kumtukuza na kumtakasa, kama wanavyosema wenyewe:Hakuna yoyote miongoni mwetu ila anapo mahali pake mahususi.
Soma Zaidi...Mwanadamu ukifikiria vyema. Kuhusu nafsi yako, hakika utapatabfikra yabuwepp wa Mwenyezi Mungu
Soma Zaidi...Mahusiano kati ya elimu ya mwongizo na elimu ya mazingira katika uislamu.
Soma Zaidi...Ilhamu ni moja katika njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu na kuwafundisha mambo mablimbali.
Soma Zaidi...Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.
Soma Zaidi...Ukweli ni katika sifa za waumini. Siku zote hakuna hasara katika kusema ukweli. Kinyume chake uongo ni katika madhambi makubwa sana.
Soma Zaidi...Nao husema (kwa maskhara): "Je, tutakapopotea katika ardhi, (tukageuka mchanga) ndio tutarudishwa katika umbo jipya?
Soma Zaidi...