picha

Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili

Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili

Kujiepusha na ubadhirifu (israfu) na ubakhili


(b)Kujiepusha na Ubadhirifu (israfu)


Ubadhirifu ni utumiaji wa mali au kitu chochote kile chenye thamani kama vile muda, zaidi kuliko mahitajio. Pia kutoa mali au huduma na kuwapa watu wasiostahiki ni katika kufanya ubadhirifu. Vile vile kutumia mali au muda katika yale yaliyoharamishwa, ni katika israfu. Ubadhirifu wa aina zote umekatazwa katika Uislamu na afanyae ubadhirifu ni rafiki yake shetani.



(c)Kujiepusha na ubakhili
Ubakhili ni kinyume cha ubadhirifu.Ubakhili ni kitendo cha kuwanyima msaada wale wanaostahiki wakati uwezo wa kuwasaidia upo. Pia ni katika kufanya ubakhili kwa mtu kujinyima mahitaji muhimu ya maisha kama vile lishe bora, mavazi na makazi bora na huku anauwezo. Katika kutumia na kutoa misaada, Waumini wanatakiwa wawe kati na kati:


"Wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika ”(17:29)



"Na (katika waja wa Rahman ni) wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa kati kati baina ya hayo." (25:67)




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views 2283

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 ai web app     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 web hosting     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

Taqwa (Hofu ya kumuogopa Allah) ni popote ulipo

عَنْ أَبِي ذَرٍّ جُنْدَبِ بْنِ جُنَادَةَ، وَأَبِي عَبْدِ الرَّحْمَنِ مُعَاذِ بْنِ جَبَلٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، عَنْ رَسُولِ اللَ...

Soma Zaidi...
NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)

Zifuatazo ni njia nyingi za kumjua Mwenyezi Mungu (EDK form 2:dhana ya elimu katika uislamu)

Soma Zaidi...
Kumuamini mwenyezi Mungu (S.W)

Nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...