Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo.
Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Hata kama mtu amefanya kosa la kustahiki kuuliwa, hatauliwa kwa mtu binafsi kuchukua sharia mkononi bali itabidi afikishwe mbele ya Kadhi na ahukumiwe kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.
Si nafsi ya binaadamu tu iliyoharamishwa kuuliwa pasina haki bali hata nafsi za viumbe vingine vyote ikiwa ni pamoja na wanyama wakubwa na wadogo na mimea. Kwa mfano tunaruhusiwa kuwaua wanyama kwa ajili ya manufaa kutoka kwao au kwa ajili ya kujikinga na madhara yao dhidi ya binaadamu. Pia haturuhuswi kukata au kuteketeza mimea ovyo ovyo pasina haja maalumu na kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
β Wala msiwaue watoto umasikiniβ¦β(1 7:31)
Kiutendaji kuwaua watoto kwa kuogopa umasikini si lazima kuishia kwenye kuwaua watoto waliokwisha zaliwa bali hata kuzuia mimba isitokee, kutoa mimba au kufunga kizazi bila ya sababu ya msingi ya kiafya ni katika kuua watoto. Na katika aya hizi Allah (s.w) anatahadharisha:
"β¦ Kwa yakini kuwaua ni khatia kubwa". (17:31)
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Allah hutumia maandishi kuwafundisha wanadamu. Mfano mzuri ni nabii Musa ambaye alipewa vibao vya maandishi.
Soma Zaidi...Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu katika uislamu? Nini naana ya elimu ya muongizo. Je elimu ya mazingiravmaana yakeni nini. Ni upi utofauti wa elimu ya muongozo na elimu ya mazingira?
Soma Zaidi...Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini? (EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo)
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...