Kuua nafsi bila ya Haki, ni kuiua nafsi isiyo na kosa linalostahiki hukumu ya kifo. Hata kama mtu amefanya kosa la kustahiki kuuliwa, hatauliwa kwa mtu binafsi kuchukua sharia mkononi bali itabidi afikishwe mbele ya Kadhi na ahukumiwe kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu.
Si nafsi ya binaadamu tu iliyoharamishwa kuuliwa pasina haki bali hata nafsi za viumbe vingine vyote ikiwa ni pamoja na wanyama wakubwa na wadogo na mimea. Kwa mfano tunaruhusiwa kuwaua wanyama kwa ajili ya manufaa kutoka kwao au kwa ajili ya kujikinga na madhara yao dhidi ya binaadamu. Pia haturuhuswi kukata au kuteketeza mimea ovyo ovyo pasina haja maalumu na kwa kuzingatia utunzaji wa mazingira.
“ Wala msiwaue watoto umasikini…”(1 7:31)
Kiutendaji kuwaua watoto kwa kuogopa umasikini si lazima kuishia kwenye kuwaua watoto waliokwisha zaliwa bali hata kuzuia mimba isitokee, kutoa mimba au kufunga kizazi bila ya sababu ya msingi ya kiafya ni katika kuua watoto. Na katika aya hizi Allah (s.w) anatahadharisha:
"… Kwa yakini kuwaua ni khatia kubwa". (17:31)