image

Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu

Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira.

Kwa mtazamo wa Uislamu (Qur-an na Sunnah) hapana mgawanyo huu wa elimu kwa sababu za msingi zifuatazo:


Kwanza, Nabii Adam (a.s) katika kuandaliwa yeye na kikazi chake kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni alifundishwa majina ya vitu vyote kama Qur-an inavyoainisha:

 


“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote…” (2:31).
Majina ya vitu vyote hapa kama tulivyotangulia kusema inaashiria fani zote za elimu zitakazomuwezesha binaadamu kuendea kila kipengele cha maisha yake na kufikia malengo tarajiwa.

 

Pamoja na kufundishwa majina ya vitu vyote, pia Adam (a.s) na kizazi chake waliahidiwa na Mola wao kuletewa mwongozo utakaowawezesha kutumia fani mbali mbali za taaluma walizonazo kwa kufuata utaratibu utakaowapelekea kukiendea kila kipengele cha maisha yao kwa furaha na amani:


“Tukasema: Shukeni humo nyote; na kama ukikufikieni uwongozi utokao kwangu, basi watakaofuata uwongozi wangu huo, haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.” (2:38).

 


Lakini wale watakaotumia taaluma mbali mbali walizonazo katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii bila ya kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na Vitabu vyake, wataishi maisha ya huzuni na khofu na katika maisha ya akhera watakuwa na adhabu kali:
“Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watakaokuwa watu wa motoni, humo watakaa milele.” (2:39)

 

Kwa mujibu wa maelezo haya tunajifunza kuwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) ambazo amezifundisha Allah (s.w) pamoja na mwongozo maalumu kutoka kwake, vinahitajika kwa binaadamu ili kumuwezesha kuishi maisha ya furaha na amani hapa duniani na huko akhera.

 

Hivyo hapana mwenye uwezo wa kutenganisha maisha ya dini na dunia au elimu ya dini na dunia.

 


Pili, Amri ya kusoma (kutafuta elimu) aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake, haibagui elimu ya dini na dunia.

 

Vinginevyo fani yoyote ya elimu inayomuwezesha binaadamu kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii na kufikia lengo la kuumbwa la kumuabudu Allah (s.w) inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake inapaswa isomwe kwa juhudi zote.

 


Tatu, chanzo cha fani zote za elimu ni Allah (s.w) kama Qur-an inavyosisitiza:

 

“Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha (Binaadamu fani zote za elimu) kwa msaada wa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya mambo) aliyokuwa hayajui”. (96:3-5)
Kwa mujibu wa aya hizi hapana fani yoyote ya taaluma iliyoasisiwa na binaadamu. Hivyo suala la kuwa na elimu ya dunia iliyoasisiwa na binaadamu na elimu ya dini ambayo tu ndiyo iliyotaka kwa Allah (s.w), halipo kwa mtazamo wa Qur-an.

 


Nne, katika Qur-an tunafahamishwa kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo na kumuogopa ni wale wataalamu (ulamaa) waliozama katika fani mbali mbali za elimu. Kwa mujibu wa Qur’an fani hizi mbali mbali haziishii tu kwenye zile fani zinazotazamwa kwa mrengo wa kidini kama vile fiqh, Tawhiid, n.k. bali fani zote za elimu zinazo muwezesha binaadamu kutafakari kwa undani juu ya kuwepo Allah (s.w) na daraja ya utukufu wake, hasa zile fani za kisayansi zinazohusiana na maumbile. Hebu turejee aya zifu atazo:

 


Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji toka mawinguni! Na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana. (35:27)

 

Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali. Kwa hakika wanaomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanavyuoni). Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Msamehevu. (35:28).

 

Katika aya hizi tunajifunza kuwa wenye kumcha Allah (s.w) ipasavyo na katika kiwango cha juu cha unyenyekevu ni wale waumini waliobobea katika taaluma mbali mbali (maulamaa).

 

Je, maulamaa waliotajwa katika aya hizi ni wale tu waliobobea kwenye taaluma zinazoitwa za kidini kama vile fiq-h, Qur-an na Hadith? Maulamaa waliopigiwa mfano katika aya hizi ni wale waliozama katika fani ya Hali ya Hewa (Meteorologist), Maulama waliozama katika uchunguzi wa wanyama (Zoologist), maulamaa waliozama katika fani ya matunda (Horticulturist), Maulamaa waliozama katika fani ya Madini (Geologists) na Maulamaa waliozama katika fani ya kuchunguza watu walivyo kimaumbile, rangi, n.k. (Anthropolagist).

 

Pia katika aya nyingi za Qur-an binaadamum amesisitizwa kuyafanyia utafiti mazingira ya mbingu na ardhi ili kumtambua Mola wake na kumuabudu ipasavyo.

 

Tano, katika Qur-an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini waliobobea kwenye elimu wana daraja kubwa zaidi kuliko waumini wengine:

 

“… Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu; na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote.” (58:11)
Aya hii haijabagua wenye elimu.

 

Hivyo yeyote yule mwenye taaluma inayomuwezesha kumcha Mola wake na kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake na ikamuwezesha kuchangia katika kusimamsiha Uislamu katika jamii atakuwa na daraja zaidi kuliko wale wasio na taaluma hiyo kama Qur-an inavyozidi kusisitiza:

 

“… Hakika ahishimiw aye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mw enyezi Mungu zaidi katika nyinyi.” (49:13)


Sita, hatuoni mgawanyo wa elimu katika Hadith mbali mbali za Mtume (s.a.w) zinazozungumzia elimu. Kwa mfano Mtume (s.a.w) aliposema: “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume na kila Mu is lamu mwanamke.

 

” (Ibn Majah), hakubagua elimu. Pia rejea Hadith zifuatazo:
Anas (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mw enye kutoka nje kutafuta elimu yuko katika njia ya Allah mpaka atakapo rejea. (Tirmidh).

 

Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema:Yeyote atakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi (mkanda) wa Moto siku ya Kiyama.” (Ahmad, Abu Daud, Tirmidh na Ibn Majah).

 


Pia tunajifunza katika historia kuwa Mtume (s.a.w) aliwaacha huru mateka wa vita vya Badr kwa yule aliyeweza kujikomboa kwa kuwafunza kusoma na kuandika watoto kumi wa Waislamu.

 

Hadith hizi zinadhihirisha kuwa Mtume (s.a.w) naye hakuigawanya elimu katika elimu ya dini na elimu ya dunia. Bali Mtume (s.a.w) amewahimiza Waislamu kutafuta elimu yenye manufaa kwa jamii popote pale inapopatikana.


“Tafuteni elimu hata China” (Baihaqi).
Laiti kama pangelikuwepo na mgawanyo wa elimu na kuwa elimu ya lazima kutafutwa na Waislamu ni ile iitwayo “elimu ya dini” kwanini Mtume (s.a.w) aliwaamuru waende China wakati wahay ulikuwa unamfuata yeye alipo? Ilikuwa inatosha wao kubaki na Mtume Makkah au Madina na asiwatume tena kwenda China kutafuta elimu.


Hivyo, kutokana na hoja hizi sita, Uislamu hautambui mgawanyo wa elimu kwenye tapo la elimu ya dini na elimu ya dunia.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 898


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Nguzo za imani
Zifuatazo Ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Makundi ya dini za wanaadamu
Kwenye kipengele hichi tutajifunza makundi ya dini za watu. Na makundi hayo ni matatu. Soma Zaidi...

mitume
Labda itaulizwa: Kwanini Mtume Muhammad (s. Soma Zaidi...

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)
1. Soma Zaidi...

Maana ya Kumuamini Allah (s.w) katika Utendaji wa kila siku
Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu. Soma Zaidi...

Kuongea na Allah (s.w) nyuma ya Pazia
Hii ni njia ambayo mwanaadamu huongeleshwa moja kwa moja na Allah (s. Soma Zaidi...

Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za waumini zilizotajwa katika surat ash-Shuura
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele). Soma Zaidi...

mwanadamu hawezi kuishi bila ya Dini
Soma Zaidi...

Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...