Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.
NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:
1 Kumuamini Allah (s.w).
2 Kuamini Malaika wake.
3 Kuamini Vitabu vyake.
4 Kuamini Mitume wake.
5 Kuamini Siku ya mwisho.
6 Kuamini Qadar yake.
Hawi Muumini wa Kiislam yule ambaye amekanusha angalau moja ya nguzo hizi kama inavyobainika katika Qur-an:
“... Na mwenye kumkanusha Allah (s.w) na Ma la ika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho., basi bila shaka amepotea upotofu ulio mbali (kabisa)” (4:136)Mtu hatakuwa Muumini kwa kutamka tu hizi nguzo sita, bali pale atakapozijua kwa undani na kuendesha maisha yake yote kwa misingi ya nguzo hizi.
Tunazifahamu nguzo hizi sita kutokana na Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosimuliwa na Umar (r.a) kama ifuatavyo:Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.aw.) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote.
Halafu alikaa mbele ya Mtume (s.a.w) hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume na akasema:”Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu ” na Mtume akasema ; “Ni kushuhudia ya kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Kusimamisha swalaa, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkat kwa mwenye kuweza” Halafu yule mgeni akasema “umesema kweli”. Tukastaajabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha.
Halafu akasema; “Nifa ham ishe juu ya Iman ”. Mtume akasema : “Ni kumuamini Mwenyezimungu na, Ma la ika wake , Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri na shari yake.
Kisha akasema nifahamishe juu ya Ihsaan” Akasema “Ni Kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni yeye anakuona ” Halafu akasema nifahamishe juu ya Kiyama ” Akasema: “Hajui mwenye kuulizwa juu ya hilo zaidi ya mwenye kuuliza.
Akasema “Nifahamishe dalili zake. Mtume akasema: “Ni wakati ambapo mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapowaona wachungaji masikini wanaposhindana kujenga maghorofa. “Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda kisha akasema: “eweUmar, unamfahamu muulizaji?’ Sote tukamjibu kuwa Allah na Mtume wake wanajua zaidi. Mtume akasema “Huyo ni Jibriil amekuja kuwafundisheni dini yenu” (MUSLIM)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
“Basi vyote hivi mlivyopewa ni starehe ya maisha ya dunia tu, lakini kilicho kwa Mwenyezi Mungu ni bora na cha kudumu (milele).
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi titajifunza maana ya uislamu,na maana nyingine tofauti.
Soma Zaidi...Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira.
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Ni kipi chanzo cha Elimu, na ni kwa namna gani Allah hufundisha Elimu kwa wanadamu?
Soma Zaidi...Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo.
Soma Zaidi...