Mtazamo wa makafiri juu ya dini
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Mtazamo wa Makafiri juu ya Dini.
Mtazamo wa kikafiri juu ya dini uko katika sehemu kuu tatu zifuatazo;
Maana ya dini.
Chimbuko, Asili au Chanzo cha dini.
Kazi ya dini katika jamii.
Maana ya dini.
Ni imani juu ya kuwepo Mungu Muumba Muweza na Mwenye nguvu juu ya kitu.
Rejea tafsiri ya neno Religion katika Kamusi ya Kiingereza.
Belief in the existence of a supernatural ruling power the creator …..”
Tafsiri:
Dini ni imani ya kuwepo Mungu Muumba aliyemuweza na mwenye nguvu..
Chimbuko, Chanzo au Asili ya dini.
Makafiri wanadai kuwa chimbuko la dini linatokana na mawazo na fikra finyu za mwanaadamu alipokuwa katika maisha ya ujima (primitive age).
Dini ni fikra na dhana alizoibua mwanaadamu baada ya kushindwa kutatua matatizo ya kijamii, uchumi, siasa, n.k.
Dini ni dhana iliyoibuliwa na mwanaadamu kutokana na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Rejea kitabu cha Kafiri, F. Angels kiitwacho Anti-Duhring
“Religion arose from primitive conceptions of men
Tafsiri:
Dini imeibuka kutokana na ujima (uduni) wa mawazo ya mwanaadamu
(c) Kazi ya dini katika jamii.
Ukirejea historia ya Ulaya na nchi za Magharibi, Kanisa kama dini lilitumika kwa kazi zifuatazo;
- Ni chombo kinacholeta unyonyaji, ukandamizaji na dhuluma katika jamii.
Rejea Quran (28:4).
Ni chombo cha kuleta matabaka na ubaguzi kati ya viongozi (mabwana) na waongozwa, matajiri na masikini katika jamii.
Pia dini inaaminika kuwa ni chombo cha kulinda na kutetea maslahi ya watawala kupitia mafundisho yake.
Dini inatumika kama chombo cha kuchuma na kujilimbikizia mali kwa wakuu (viongozi) wake kwa kuwatumia wafuasi wake.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Madrasa kiganjani ๐2 kitabu cha Simulizi ๐3 web hosting ๐4 Kitau cha Fiqh ๐5 Kitabu cha Afya ๐6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
UMBILE LA MBINGU NA ARDHI
โKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.
Soma Zaidi...Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini.
Soma Zaidi...Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Njia ambazo Allah hutumia kuwasiliana na wanadamu nakuwafundisha elimu mbalimbali. (Edk form 1 dhana ya Elimu)
Soma Zaidi...ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU
ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ู ููู ููุงูู ููุคูู ููู ุจูุงููููููู ููุงููููููู ู...
Soma Zaidi...Mgawanyiko wa Elimu katika mtazamo wa Uislamu
Katika Uislamu elimu imegawanyika katika Elimu ya muongozo na elimu ya mazingira.
Soma Zaidi...Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu
Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)
Soma Zaidi...