Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Yanayochochea zinaa ni pamoja na mavazi yasiyozingatia sheria ya Kiislamu; michanganyiko ya wanaume na wanawake isiyozingatia sheria ya Kiislamu; michezo, miziki, ngoma, nyimbo na mengineyo yanayochochea zinaa.
"β¦ Hakika hiyo zinaa ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa)" (17:32)
Uchafu na ubaya wa zinaa unadhihirika wazi kwa wahusika binafsi na kwa jamii kwa ujumla katika maeneo yafuatayo:
(i)Magonjwa ya zinaa ukiwemo UKIMWI, ambayo hudhoofisha afya na kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi na maendeleo ya jamii kwa ujumla.
(ii)Kuporomosha maadili ya jamii. Watu wazinifu hawana haya, ni watovu wa nidhamu, walaghai, waongo, wabinafsi na wapupia machafu ya kila namna.
(iii)Zinaa huondosha umuhimu na heshima ya ndoa.
(iv)Kuvunja ndoa na kusababisha matatizo ya kifamilia.
(v)Husababisha watoto wa mitaani na kuingiza jamii katika janga la wahuni, wala unga, matapeli, majambazi pamoja na kusababisha kundi kubwa la vijana wasio na uwezo wa kufanya lolote.
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika Qur'an tunakumbushwa neema mbali mbali walizotunukiwa Bani Israil (Mayahudi) na Mola wao ili kuwawezesha kusimamisha Ufalme wa Allah(s.
Soma Zaidi...Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.
Soma Zaidi...Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...