(b)Kujiepusha na Ubadhirifu (israfu)
Ubadhirifu ni utumiaji wa mali au kitu chochote kile chenye thamani kama vile muda, zaidi kuliko mahitajio. Pia kutoa mali au huduma na kuwapa watu wasiostahiki ni katika kufanya ubadhirifu. Vile vile kutumia mali au muda katika yale yaliyoharamishwa, ni katika israfu. Ubadhirifu wa aina zote umekatazwa katika Uislamu na afanyae ubadhirifu ni rafiki yake shetani.
(c)Kujiepusha na ubakhili
Ubakhili ni kinyume cha ubadhirifu.Ubakhili ni kitendo cha kuwanyima msaada wale wanaostahiki wakati uwezo wa kuwasaidia upo. Pia ni katika kufanya ubakhili kwa mtu kujinyima mahitaji muhimu ya maisha kama vile lishe bora, mavazi na makazi bora na huku anauwezo. Katika kutumia na kutoa misaada, Waumini wanatakiwa wawe kati na kati:
"Wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako, wala usiukunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika ”(17:29)
"Na (katika waja wa Rahman ni) wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa kati kati baina ya hayo." (25:67)
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hichi tutajifunza mitazamo ya kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...