Kwa nini katika uislamu elimu imepewa nafasi ya kwanza ( EDK form 1 Dahana ya elimu)
Kwa nini Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
1. Ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake na kuweza kumuabudu ipasavyo.
“Kwa hakika wanaomuogopa (wanaomuabudu) Mwenyezi Mungu ipasavyo miongoni mwa waja wake ni wale wataalamu” (35:28).
2. Elimu iliyosomwa kwa murengo wa Qur’an na Sunnah ndio inayomuwezesha muumini kuwa Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni.
“Na kumbukeni aliposema Allah kuwaambia Malaika kwamba ataweka ardhini khalifa (kiongozi)” (2:30) pia rejea (2:38).
3. Kutafuta elimu ni ibada maalum yenye hadhi kubwa kuliko ibada zote mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) inayopelekea mja kufanya ibada vilivyo.
“……Na (waumini) waliopewa elimu watapata daraja (kubwa) zaidi…” (58:11).
4. Mwenye elimu ndio ana nafasi bora ya kumtambua na kumuabudu Mola wake ipasavyo kwa kila kipengele cha maisha yake.
Rejea Qur’an (35:28), (39:9) na (58:11).
Umeionaje Makala hii.. ?
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake.
Soma Zaidi...Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.
Soma Zaidi...