Makala hii inakwenda kukueleza kuhusu fati, vyakula vya fati, kazi zake na athari za upungufu wake
FATI, MAFUTA NA LIPID
Fati ni moja kati ya virutubisho vikuu vitatu ambavyo ni wanaga an protini. Fati imetengenezwa na chembechembe za kaboni na haidrojen. Fati, mafuta na lipid ni maneno mawili yanayohusiana lakini kuna utofauti kidogo. Tunaposema lipid tunamaanisha fati na mafuta. Tunaposema fat tunamaanisha lipid iliyo katika hali ya yabisi (kitu kigumu) na tunaposema mafuta ni lipid iliyo katika hali ya kimiminika. Lakini mara nyingi tunaposema fati tunajumuisha vyote yaani lipi na mafuta.
Kazi za fati mwilini
1. Husaidia katika utengenezwaji wa nishati mwilini
2. Husaidia katika kuipa joto miili yetu
3. Husaidia katika kulinda sehemu za ndani za miili yetu
4. Husaidia katika utoaji wa taarifa mbalimbali ndani ya mwili
5. Husaidia protini kufanya kazi zake vyema
6. Husaidia katika ukuaji wa kiumbe
7. Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga mwilini
8. Husaidia katika mfumo wa uzalianaji
Vyakula vya fati
1. Mapalachichi
2. Siagi
3. Maziwa
4. Mayai
5. Karanga na jamii za karanga kama korosho
6. Mbegu za chia
7. Samaki
8. Choklet
9. Nazi
10. Nyama
11. Maharagwe ya soya
12. Alizeti
Upungufu wa fati
1. Kukauka kwa ngozi na ukurutu
2. Mupata maambukizi ya mara kwa mara
3. Kupona kwa vidonda kuliko hafifu
4. Kuchelewa kukua cha watoto
Umeionaje Makala hii.. ?
tangawizi ni katika viungio vya mboga vyenye faida, pia ni kinywaji, zijuwe leo faida za tangawizi
Soma Zaidi...Hivi ni vyakula hatari kwa vidonda vya tumbo. mwenye vidonda vya tumbo hatakiwi kula vyakula hivi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi vitamini mbalimbali na kazi zake kwenye mwili,vitamini ufanya kazi mbalimbali kwenye mwili kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...