Somo hili linakwenda kukuletea matunda yenye vitamin C kwa wingi
MATUNDA YENYE VITAMINI C KWA WINGI
Vitamini C ni katika vitamini ambavyo wili unavihitajia kwa wingi kwa lengo la kuboresha mfumo wa kinga mwilini. Tunaweza kupata vitamini hivi sana kutoka kwenye matunda. Katika makala hii nitakwenda kukutajia matunda aina 7 ambayo yana vitamini c kwa wingi sana.
Aina ya matunda yenye vitamini C
1.Embe, embe linafahamika kwa utamu wake na uchachu wake. Vitamini C vinapatikana kwa wingi zaidi kwenye matunda yenye uchachu.
2.Mapera; tunda hili limeenea maeneo mengi, kula pera likiwa limewiva ama likiwa limekomaa na tayari kulila.
3.Papai, mapapai ni katika matunda mabyo yana rangi ya njano. Matunda haya yana sifa ya kuwa na vitamini hivi kwa wingi
4.Karoti, kitaalamu karoti si tunda. Lakini nimependa kuliweka kwenye orodha hii kwa sababu watu hutafuna karoti na kuifanya kama tunda.
5.Limao na ndimu, hapa ndipo penyewe kwa vitamini C. limao na ndimu ndio matunda yenye uchachu kwa wingi na hivyo kukusanya vitamini C.
6.Nanasi, tunda hili pia ni katika matunda yenye rangi ya njano. Sifa hii hufanya tunda hili liwe miongoni mwa vyanzo vikuu vya vitamini C.
7.Chungwa, machungwa yana faida nyingi mwilini ikiwemo kutupatia vitamini C kwa wingi.
8.Nyanya, pensheni, palachichi, tufaha na pilipili haya ni katika matunda mengine yenye vitamini C kwa wingi kabisa.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi faida za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito, kuna kipindi ambacho wanawake wakati wa ujauzito uchaguza vyakula mbalimbali kuna ambao wanaweza kutumia vitunguu saumu na kupata faida kubwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi magonjwa nyemelezi kwa watoto wadogo chini ya miaka mitano,. Ni magonjwa yanayowapata watoto wadogo kwa sababu kinga Yao bado ni ndogo.
Soma Zaidi...Nashukuru kwa ushauri, Je!
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukueleza faida za kula maboga, na mbegu zake kwa afya yako
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kufundisha vyakuna na vinjwaji salama anavyopaswa kutumia mgonjwa wa vidonda vya tumbo. Pia utajifunza vyakula na vinywaji hatari kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo.
Soma Zaidi...