Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vya hatari kwa mjamzito hasa mimba changa
VYAKULA HATARI KWA MJAMZITO HASA KWA MIMBA CHANGA
1.Mayai mabichi: Mayai ni chakula kizuri kila mtu anatambuwa hili. Hata hivyo si jambo jema kula mayai mabichi. Hii inaweza kuwa hatari kwa ujauzito hasa kwa mwenye ujauzito mchanga. Hivyo epuka kula mayai mabichi ama yasiyowiva vyema.
2.Maini ya wanyama kwa wingi: Maini ni katika vyakula ambavyo vina virutubisho vingi sana. Kama ijulikanavyo ini lina kazi nyingi mojawapo ni kuondoa sumu mwilini. Hivyo unahitajika kutokula maini kwa mjamzito.
3.Shubiri: shubiri hufahamika kwa uchungu wake. kwa mwenye ujauzito hasa mimba changa shubiri sio salama. Shubirilinaweza kutoa ujauzito kama litatumika kwa kulinywa. Onyo hili linaandamana na miti mingine michungu.
4.Viazi mbatata vilivyoanza kuota: onyo hili ni kwa nafaka zote zinazoanza kuota sio nzuri kula. Hasa hasa viazi mbatata ambavyo vimeanza kutoa miche sio salama kwa mwanamke mjamzito kutuia kama chakula.
5.Mapapai hasahasa mapapai yasiyowiva: Matunda nimuhmu sana kwa mjamzito kwa afya yake na ya mtoto wake. Hata hivyo kuna matunda sio mazuri kuyala kwa wingi kwa mwenye mimba changa. Mapapai ni mojawapo, hasa papai ambalo halikuwiva, yaani lile la kijani lililokomaa.
6.Mananasi: nanasi ni kama papai, kama mjamzito atatumia kwa wingi, inaweza kuwa hatari kwa mimba iliyochanga.
7.Vyakula ambavyo havijawiva vyema hususani samaki na nyama: sio samaki tu na nyama, chakula chochote ambacho hakikuwiva vyema ni hatari sana kwa mwenye uauzito. Hii ni sawa na nyama ya kuku na vyakula vingine.
8.Kutumia majani ya chai yenye caffein kwa wingi. Mjamzito hakatazwi kunywa chai ya majani ya chai. Kilichokibaya ni kuzidisha unywaji wa chai yenye majani ya chai kupitiliza. Majani ya chai yana kemikali inayoitwa caffein, hii ikiwa nyingi inakuwa hatari kwa ujauzito.
9.Chumvi kwa wingi10.Energy drink
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Some Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia kuhusiana na dalili za upungufu wa iodini ambapo kitaalamu hujulikana Kama goiter. Goiter Ni Sababu ya kawaida ya goiter duniani kote ni ukosefu wa iodini katika chakula. Nchini Marekani, ambako utumiaji wa chumvi yenye iodini ni j
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za mchaichai
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za mchai chai, ni mmea ambao upandwa na watu kama maua, dawa au kikolezo cha chai na Kuna wengine kabisa wanatumia kama sehemu Mojawapo ya dawa kwa hiyo tutaona faida za mmea huu wa mchai chai.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula panzi senene na kumbikumbi
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant)
Soma Zaidi...