Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu

Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu

Kazi na Wajibu wa KhalifaKhalifa katika Serikali ya Kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali kama alivyokuwa Mtume(s.

Download Post hii hapa

Kazi na wajibu wa khalifa katika dola ya kiislamu

Kazi na Wajibu wa Khalifa
Khalifa katika Serikali ya Kiislamu ndiye mtendaji mkuu wa Serikali kama alivyokuwa Mtume(s.a.w). Akiwa mtendaji mkuu wa Serikali, kwa ujumla Khalifa atasimamia utekelezaji wa madhumuni ya kuwepo Dola ya Kiislamu ambayo ni


(1) Kuhuisha, kuendeleza na kudumisha maadili mema ambayo hupelekea watu katika jamii kuishi kwa furaha na amani.


(2) Kuzuia na kukomesha maovu ambayo huleta vurugu, mashaka na huzuni katika jamii, Wale ambao tukiwamakinisha, (tukiwaweka uzuri) katika ardhi husimamisha Sala na wakatoa Zaka na wakaamrisha yaliyo mema na wakakataza yaliyo mabaya. Na marejeo ya mambo ni kwa Mwenyezi Mungu. (22:41)



Katika kutekeleza madhumini haya ya Dola ya Kiislamu, Khalifa aliwajibika kufanya yafuatayo:


(i) Kujenga maisha ya binaadamu juu ya msingi wa ucha- Mungu na matendo mema. Kuyasafisha maisha ya binaadamu kutokana na maasi, kudumisha haki na usawa, kukomesha ukatili, ukandamizaji, utabaka, uonevu,unyonyaji, udhalimu n.k.


“Kwa hakika tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na kuteremsha vitabu na uadilifu pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu..............” (57:25)


(ii) Kutumia uchumi wa Taifa kwa kukuza na kuendeleza maadili mema kwa raia wake.


(iii) Kuamrisha mema na kukataza mabaya. Hatua nne zilichukuliwa katika kufanikisha jukumu hil:


(a) Kuteua mahakimu wacha-Mungu wa kusimamia haki na sheria.


(b) Kuteua Madai’yah (Waalimu) wa kuwaelekeza watu yepi mema na namna ya kuyaendea na yepi maovu na namna ya kuyaepuka.


(c) Hutuba za Ijumaa, Idd na Hijja zilitumika kukazia wema na ucha-Mungu.


(d) Kuteua tume ya kufuatilia tabia za watu na kuadhibu hapo hapo kwa makosa yasiyohitaji kwenda mahakamani.


(iv)Kulinda mipaka ya dola kwa gharama yoyote. Mipaka ya Dola ililindwa ama kwa vita au kwa diplomasia.


(v) Pamoja na kulinda na kutekeleza madhumuni ya dola ya Kiislamu, Khalifa akishirikiana na Shura yake, aliteua viongozi mbali mbali wa Serikali ikiwa ni pamoja na wakuu wa majimbo (Walii au Gavana), Mahakimu,(Makadhi)wakusanya kodi,(maamil) majemedari,makatibu, wakuu wa polisi, n.k.


Kwa mfano Khalifa Abubakar aliteua magavana 17 kuongoza majimbo (mikoa) 17 ya Serikali yake. Naye ‘Umar aliteua Magavana 15 katika Serikali yake.


(vi)Khalifa alikuwa ndiye mkuu wa majeshi. Aliamuru vita vipiganwe au visipiganwe, alisaini mikataba, aliteua maamiri jeshi na kupeleka maelekezo katika uwanja wa vita. Abubakar na Ali waliongoza mapigano kama Mtume(s.a.w) alivyofanya, lakini ‘Umar na ‘Uthuman hawakujaaliwa fursa hii lakini wamekufa mashahidi kwa kuuliwa na wapinzani.


(vii)Khalifa alikuwa ndiye mwanasheria mkuu wa Serikali.
Alisikiliza kesi na kutoa hukumu na yeye ndiye aliyekuwa mahakama ya rufaa. Mikoani waliteuliwa makadhi walioendesha kesi na kutoa hukumu kwa niaba yake.


Malipo ya Khalifa



Abubakar alipochaguliwa kuwa Khalifa aliendelea na kazi yake ya biashara. Alipokuwa anakwenda sokoni kuuza nguo alikutana na Umar na Abu Ubaida ambao walimkataza. Ndipo shura ikakaa na kuamua kuwa apewe kiwango maalum cha posho kutoka katika Baitul-Mali cha kumuwezesha kuishi maisha ya kawaida. Zaidi ya kasma hii hakuruhusiwa kuchukua zaidi. Hata hivyo Khalifa Abubakar alirudisha kwenye Baitul Mali posho yote aliyopewa kutokana na maelekezo yake alipokuwa anafariki Dunia. Katika Ukhalifa wa Umar mishahara ilipangwa kwa wafanyakazi na viongozi wa Serikali. Hivyo Khalifa Umar na Ali walichukua posho zao ila Uthman alitumia pesa zake kwa vile alikuwa na uwezo wa kiuchumi.




                   


Download Post hii hapa

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1427

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Ni jitihada gan alizo zifanya sayyidna othman katika kuihifadh qur an ?
Ni jitihada gan alizo zifanya sayyidna othman katika kuihifadh qur an ?

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu Jitihada alizozifanya Khalifa wa Tatu katika kuilinda Quran

Soma Zaidi...
Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)
Maryam Apewa Habari ya Kumzaa Isa(a.s)

Baada ya maandalizi hayo ya kimalezi pamoja na hifadhi ya Allah(s.

Soma Zaidi...
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
tarekh 08
tarekh 08

KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s.

Soma Zaidi...
Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.
Kujengwa upya al Kabah baada ya kuwa na mipasuko.

Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba 🕋

Soma Zaidi...