image

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri

Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji.

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri

Yusufu Aokotwa na Kuuzwa nchini Misri


Huko nyuma wapita njia walikisogelea kisima kwa lengo la kuteka maji. Mmoja wao katika harakati za kuteka maji,alimuibua mtoto akaruka kwa mshangao:



..........Akasema: Ee,furaha njema! Huyu hapa kijana mwanaume.............. (12:19) Walimchukua hadi Misri na kumuuza kwa Al-Aziz au Waziri,



Wakamuuza kwa thamani chache ya pesa za kuhesabika, na hawakuwa na haja naye (12:20)

Yusufu(a.s) Apewa Utume na Kukumbana na Mtihani Alipofikia umri wa utu uzima alipewa hukumu na elimu. Yaani akapewa Utume. Qur’an inasema:-

“Na (Yusuf) alipobaleghe, tulimpa hukumu na ilimu. Na namna hivi tunawalipa wanaotenda mema” (12:22).



Katika kipindi hiki cha utu uzima mke wa Waziri alifanya vitimbi na hata kumshika Yusufu kwa nguvu ili azini naye. Lakini Yusufu alikataa kufanya tendo hilo ovu. Alipoambiwa ‘njoo’, Yusufu akasema:



Najikinga kwa Mwenyezi Mungu. Hakika yeye (mumeo) ni bwana wangu, ametengeneza makazi yangu hapa vizuri. Hakika madhalimu hawatengenekewi(12:23)



Al-Aziz, aliyemnunua Yusufu(a.s) alimwangalia vizuri kama mtoto wake wa kulea. Lakini kwa bahati mbaya,Yusufu(a.s)alipofikia baleghe mkeweAl-Aziz alimtamani na kutaka wazini naye. Yusufu(a.s)alimkatalia kwa hoja kuwa kufanya hivyo ni kumwasi Allah(s.w) na pia itakuwa ni kumfanyia khiyana Al-Aziz, ambaye amemkirimu makazi mazuri pale Misri (Rejea Qur’an 12:23).



Mkewe Al-Aziz hakutaka kusikiliza hoja za Yusfu(a.s),bali alimkazania kuwa lazima akubali kufanya kitendo hicho na akafunga mlango.

“Na (mwanamke huyo) akamkazia nia(ya kutaka kumdhuru vile alivyomkataa) na (Yusufu) akamkazia nia (ya kumpiga; akitaka kumpiga). kama (Yusufu)asingaliona dalili za (kufahamishwa na) Mola wake (kuwa kumpiga huyo mwanamke si uzuri, angelimpiga bali alikimbia tu).Tumefanya namna hivi ili Tumwepushie kila jambo la ubaya na la uovu(kama huko kuzini). Hakika yeye alikuwa katika waja wetu waliosafishwa.(12:24)



Yusufu(a.s) kwa kukwepa shari ile ilibidi akimbilie mlangoni na yule mwanamke akawa anamkimbiza na kuchana kanzu yake kwa nyuma. Kufika mlangoni wakakutana na Al-Aziz na kesi ikaanzia hapo:



Na (wote wawili) wakakimbilia mlangoni na mwanamke huyo akairarua kanzu yake kwa nyuma. Na wakamkuta mume wake mlangoni; mwanamke akasema (kumwambia mumewe katika kutia chonza za uwongo): “Hakuna malipo ya mwenye kutaka kufanya ubaya na mkeo isipokuwa kufungwa gerezani au kupewa adhabu inayoumiza”(Anamsingizia uwongo Nabii Yusufu kuwa anamtaka). (12:25)




(Yusufu) akasema: “Huyu (mwanamke) ndiye aliyenitaka bila mimi kumtaka.” Na shahidi aliyekuwa katika jamaa za huyu(mwanamke) akatoa ushahidi(akasema): “Ikiwa kanzu yake imechanwa mbele basi (mwanamke huyu amesema kweli, naye (Yusufu) yu katika waongo. “Na kama kanzu yake imechanwa nyuma, basi (mwanamke huyu) amesema uwongo, naye (Yusufu) yu katika wakweli(12:26-27)



“Basi (mumewe)alipoona kanzu yake imechanwa kwa nyuma (alijua kuwa Yusufu ndiye aliyekuwa akitaka kukamatwa kwa nguvu) akasema: “Hakika hii ni katika hila zenu wanawake; bila shaka hila zenu ni kubwa. (Wewe ndiye uliyeazimia mabaya, unakwenda kumsingizia yeye!) “Yusufu! Yaachilie mbali haya (usiyasimulie nje). Na wewe (mwanamke) omba msamaha kwa dhambi zako . Hakika wewe ni katika wanaofanya makosa. (12:28 - 29)



Mkewe Al-Aziz badala ya kujuta kwa kosa lake lile na kuleta toba, alishabikia kwa kuwaalika wanawake wengine wa mji waliomlaumu kwa kitendo chake kile kiovu cha kutaka kumbaka mtumishi wake. Aliwaalika ili na wao washuhudie uzuri wa Yusufu na kuwahakikishia kuwa yeye hataacha kumtamani Yusufu (a.s)




Na wanawake wa mji ule (wakapata habari hii) wakawa wanasema:”Mkewe waziri anamtamani mtumishi wake pasi na kutamaniwa naye. Hakika amemuathiri kwa mapenzi, Bila shaka sisi tunamuona (mke wa waziri) yumo katika upotofu ulio dhahiri. (12:30)




Basi (mkewe waziri) aliposikia msemo wao huu aliwaita (waje waone uzuri wa Yusufu wajue kuwa mwenye kurukwa na akili kwa kumpenda Yusufu hana lawama) na akawafanyia karamu na akampa kila mmoja katika wao kisu na akamwambia (Yusufu), “Tokeza mbele yao . “Basi walipomuona waliona ni kitu kikubwa kabisa na wakakata mikono yao(kwa vile visu na wenyewe hawana habari kwa kuwa wameshughulika kumtanzama tu huyo Yusufu) hakuwa huyu ila ni malaika mtukufu. (Mkewe waziri) akasema Huyu ndiye mliyenilaumia; na hakika nilimtamani kinyume cha nafsi yake, lakini akajilinda. Na kama hatafanya ninalomuamrisha, bila shaka (nitamfanyia kila vitimbi mpaka) atafungwa gerezani na atakuwa miongoni mwa madhalili (badala ya hii hishima miongoni mwa madhalili (badala ya hii hishima anayoipata. Kisha wakaingia na wale wanawake nao kuwapeleka wajumbe kumtaka)”(12:31 - 32)



Lengo la mke wa Al-Aziz lilitimia kwa kuwaonesha wanawake wa mji kuwa haipaswi kulaumiwa kwa kumtamani Yusufu.

Ikumbukwe kuwa huyu alikuwa ni mke wa mtu mkubwa. Hivyo hata wanawake walioitwa walikuwa ni wake wa wakubwa au wenye hadhi katika jamii. Wanawake hawa kudhihirisha matamanio yao, bila ya aibu, ni kielelezo cha kuanguka kwa maadili katika jamii hiyo. Yaonesha ufuska ulikuwa umechanua sana kiasi kwamba aibu haikuwa ni kitu chenye nafasi tena katika maumbile yao.



                   





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 473


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

HISTORIA YA NABII YUSUFU(A.S.): Ndoto ya nabii Yusufu
Mtume Yusufu(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII LUT(A.S) NA WATU WA SODOMA NA GOMORA
Mtume Lut(a. Soma Zaidi...

Kusingiziwa Nabii Sulaiman Uchawi
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu. Soma Zaidi...

HISTORIA YA MTUME ILYASA(A.S)
Mtume Ilyasa ni mmoja wa Mitume waliotumwa kupitia kizazi cha Bani Israil. Soma Zaidi...

Mtume amezaliwa mwaka gani?
Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake. Soma Zaidi...

Historia ya bi Khadija na familia yake na chanzo cha utajiri wake.
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 17. Historia ya Bi Khadija na familia yake. Soma Zaidi...

Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah.
Mbinu walizotumia Makafiri wa Kiqureish katika kuupinga Uislamu Makkah. Soma Zaidi...

NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE
Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA KUJENGWA UPYA KWA AL-KA'BAH (NYUMBA TUKUFU YA ALLAH)
KUJENGWA UPYA KWA AL-KA’ABAHItambulike kuwa Al-ka’abah ndio mjengo wa kwanza kujengwa duniani. Soma Zaidi...

Maana ya kusimamisha uislamu katika dini
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kufunguliwa Yusufu(a.s) Kutoka Gerezani
Yusufu(a. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SHUAIB
Soma Zaidi...