Mawazo Tofauti Kuhusiana na Uchaguzi wa Abubakar
Zipo tofauti za kimawazo kuhusiana na uchaguzi wa Khalifa wa kwanza, Abubakar(r.a.) mara baada ya kutawafu Mtume (s.a.w.).
Wapo wasemao uchaguzi ule ulifanyika katika mazingira ya kuchanganyikiwa, kwani mkutano haukuwa rasmi. Maelezo ya kundi hili yameegemea kauli zisemazo kuwa Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walistushwa na taarifa kuwa Ansar walikuwa wamekutana kwenye ukumbi wa mikutano wa Thaqifa Bani Saidah, kumchagua kiongozi anayetokana na wao ambaye
angeshika uongozi wa dola ya Kiislamu baada ya Mtume(s.a.w.). Kwa mujibu wa kauli hizo, Abubakar(r.a.) na Umar(r.a.) walilazimika kwenda kwenye mkutano huo wakiwa na dhamira ya kuzuia usiendelee, hasa ikizingatiwa kuwa Mtume alikuwa bado hajazikwa na hilo ni suala zito lilohitajia muafaka wa Waislamu wote.
Kundi jingine lina mawazo kuwa, pamoja na kuwa mkutano wa Ansar haukuwa rasmi, lakini kuchaguliwa Abubakar(r.a.) kuliwafiki, kwa kuzingatia dokezo za Mtume(s.a.w), ishara zitokanazo na Qur’an na aliyokuja kuyafanya Abubakar(r.a.) wakati wa uongozi wake, ambayo yalidhihirisha usahihi wa chaguo la mkutano wa Thaqifa Bani Saidah.
Wapo wanaosema kuwa kutokuwepo kwa watu wa nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt) katika mkutano ule, kunabatilisha zoezi zima la uchaguzi wa Khalifa wa kwanza. Maelezo ya kundi hili yanatiwa tashdid na usia, unaodaiwa kuachwa na Mtume(s.a.w.) kwa “Ahlul- Bayt” muda mfupi kabla ya kutawafu kwake; unaosema kwamba haki ya uongozi wa ummah huu baada yake ni ya “Ahlul-Bayt”. Kwa hivyo Ali(r.a.) ndiye aliyestahiki nafasi hiyo, na warithi baada yake ni wanawe Hassan na Hussein kwa kuwa ni wajukuu wa Mtume(s.a.w.). Kundi hili linadai Ukhalifa wa Abubakar(r.a.), Umar(r.a.) na Uthman(r.a.) ni batili kwa kuwa hao si katika watu wa nyumba ya Mtume(s.a.w.) na walipewa uongozi katika mikutano isiyo rasmi. Aidha hatua ya kuwafanya Makhalifa ni kudhulumu haki ya Ali(r.a.) akiwa ndugu wa Mtume.
Na kuna wasemao kwamba, kwa kuwa Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu si ya ukoo, kabila au Taifa fulani, na kwa kuwa hakuna aya katika Qur’an inayomwamrisha Mtume(s.a.w.) kurithisha dhima ya uongozi baada yake kwa watu wa nyumbani kwake (Ahlul-Bayt), basi jukumu la uongozi wa ummah limeachwa mikononi mwa waumini wenyewe. Kiongozi atachaguliwa kwa kuzingatia sifa mbali mbali zikiwemo uoni, ucha Mungu, siha n.k.
Sifa zote hizo zimpelekee kuongoza kwa haki na uadilifu. Kwa hiyo
Ukhalifa wa Abubakar, Umar na Uthman si suala la kubishaniwa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 648
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Kitau cha Fiqh
👉6 kitabu cha Simulizi
HARAKATI ZA DINI WAKATI WA MATABIINA NA TABII TABIINA
Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Isa(a.s)
Kutokana na Historia ya Nabii Isa(a. Soma Zaidi...
Kuchaguliwa kwa Makhalifa wanne baada ya kutawaf (kufariki) kwa Mtume muhammad (s.a.w)
8. Soma Zaidi...
Kuangamizwa kwa Watu wa Lut(a.s) watu wa Sodoma na Gomora
Watu wa Lut(a. Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Hud(a.s)
(i) Tuanze kulingania kwa kuonesha upweke wa Allah(s. Soma Zaidi...
Mapambano ya Dola ya kiislamu dhidi ya maadui wa kikristo (warumi) wakati wa Mtume
Soma Zaidi...
Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Darsa za Sira historia ya Mtume (s.a.w) Jaribio la 04
Soma Zaidi...
Maandalizi ya Hijra ya Mtume na Mafunzo tunayoyapata kutoka katika hijra hii
Maandalizi ya Hijra ya Mtume (s. Soma Zaidi...
MAMA YAKE MTUME MUHAMMAD (S.A.W) ANAMLEA MTUME MUHAMAD AKIWA NA UMRI WA MIAKA MINNE (4)
KULELEWA NA MAMA YAKE ALIPOFIKA MIAKA MINNEMtume (s. Soma Zaidi...
Mafunzo kutokana na vita vya badri
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Hatua mbili kuu za kushuka kwa Quran
Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...