Hadhi na haki za Mwanamke katika jamii za Mashariki ya Kati bara la arabu hapo zamani
(c) Mashariki ya kati
Uarabuni kabla ya Ujumbe wa Mtume Muhammad (s.a.w) mwanamke alionekana kitu duni na nuksi kwa jamii. Baba akipewa habari ya kuzaliwa mtoto wa kike alijinyonga nyonga na kuhuzunika sana. Wanaume walikuwa wakitafuta kila njia ya kujiokoa na aibu hiyo ya kupata mtoto wa kike. Ilikuwa kuchagua moja katika njia mbili: Ama amzike binti huyo mzima mzima akiwa hai au aendelee kuishi maisha ya aibu na fedheha kwa kumbakisha hai.
Mara nyingine wanaume walikuwa wakiwalazimisha wake zao wanapoanza mwezi wa tisa wa ujauzito wa kuchimba shimo uvungni mwa kitanda. Shimo likiwa tayari mume anamuagiza mkewe: "Ukimzaa mtoto mwanake basi haraka sana mfukie mwenyewe katika shimo hii kabla sijaja." Qur'an inatufahamisha tabia ya Waarabu dhidi ya watoto wa kike katika aya zifuatazo:
Na mmoja wao anapopewa habari ya (kuzaliwa) mtoto wa kike, husawajika uso wake, akajaa sikitiko (akawa) anajflcha na watu kwa sababu ya ha bar mbaya ile aliyoambiwa (anafanya shauri) Je, akae nayejuu yafedheha hiyo au amfukie udongoni (akiwa hai). Sikilizeni! Ni mbaya mno hukumu yao hiyo. (1 6:58-59).
Wanawake baada ya kufiwa na waume zao, walirithiwa na wanawe wa kambo au shemeji zao. Walikuwa hawaruhusiwi kuolewa tena. Qur'an inakataza tabia hii kama ifuatavyo:
Enyi mlioamini! Si halali kwenu kurithi wanawake kwa jeuri. Wala msiwazuie (kuolewa na wanaume wengine) iii mpate kuwanyang 'anya baadhiya vile mlivyo wapa... (4:19).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π2 Dua za Mitume na Manabii π3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) π4 Kitau cha Fiqh π5 ai web app π6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Kusingiziwa Nabii Sulaiman Uchawi
Pamoja na Ucha-Mungu aliokuwa nao Nabii Sulaiman watu hawakuacha kumsingizia mambo machafu.
Soma Zaidi...Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.
Soma Zaidi...Nasaba ya Mtume Muhammad S.A.W na familia yake.
Sura na historia ya Mtume Muhammad S.A.W sehemu ya 1
Soma Zaidi...Historia ya Dhulqarnain
Dhulqarnain sio jina la mtu bali cheo, maana yake ikiwa: βMwenye Pembe Mbiliβ.
Soma Zaidi...tarekh 4
KUANGAMIZWA KWA JESHI LA TEMBOTukio la pili ni lile tukio la tembo, na ilikuwa hivi:- Kiongozi mmoja wa kiyemeni aliyetambulika kwa jina la Abrah aliona waarabu kutoka maeneo mbalimbali wanafunga misafara kuelekea Makkah kwa lengo la kwenda kuhiji.
Soma Zaidi...