MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU).
Vita hivi ni vita vilivyotokea kati ya kabila la kiquraysh wakisaidiwa na Kinana kutokea makkah na kabila la Qays ‘Aylan kutokea taif. Na vita hivi vilitokea ndani ya miezi mitukufu na vilidumi kwa muda wa miaka mktano. Na mapigano halisi yalidumu kwa muda wa siku tano tu. Vita hivi vimeitwa vita vya uovu kwani vilifanyika ndani ya miezi mitukufu. Vilitokea vita hivi wakati Mtume alipokuwa na miaka kumi na tano. Na alishiriki katika vita hivi. Ijapokuwa Mtume hakupenda kushiriki vita hivi alifanikiwa kutokushiriki ndani ya siku 2 za kwanza lakini siku tatu zilizofata ilibidi ashiriki. Hakuwahi kunyanyua upanga kwa ajili ya kupigana ila alishiriki katika kuokota misahare na kuwapatia wapiganaji.
Inasemekana katika mwezi wa dhul-qada (mfunguo ilikuwa ni ada ya waarabu enzi hizo kufanya sherehe katika sehemu iitwayo Ukaz. Katika sehemu hii ndani ya masiku haya michezo mbalimbali ilifanyika kama kamari, mashindano ya kuchezea panga, kushindana kuimba mashairi, wanawake kucheza na mengineyo mengi. Pia biashara zilikuwa zikifanyika katika eneo hili. Sasa vita hivi vilitokea kwasababu ya sintofahamu iliyotokea kati ya watu wawili wafanyabiashara. Mmoja kutoka kwenye kabila la Quraysh (Makkah) na mwengine kutokea kabila la Qays ‘Aylan kutoke taif.
Sababu ni kuwa mtu mmoja kutoka katika kabila la Quraysh alikuwa na mteja, na ikatokea kuwa mfanyabiashara mwingine kutoka kabila la Qays “Aylan akawa anamfatilia mteja yuleyule. Basi ahapa ndipo pakazuka mgogoro na hatimaye Mtu kutoka kabira la quraysh akamuua yule wa kabila la Qays ‘Aylan. Watu kutoka Taif wakaandaa jeshi kuja kulipa kisasi cha ndugu yao alouliwa bila ya sababu. Watu kutoka kabila la Quraysh wakaandaa jeshi nao kwa kulinda heshima ya kabila lao. Bila ya kujali mwezi mtukufu ambao ni haramu kumwaga damu au kupigana, na bila ya kujali sheria zao juu ya mtu aliuliwa kwa makusudi sheria inasemaje. Wakaamuwa kupigana vita kali sana.
Vita vilianza mwanzoni mwa siku na toka vinaanza ushindi ulikuwa ni kwa kabila la Qaysh ‘Aylan lakini ilipofika mida ya jioni meza ikabadilika na ushindi ukawa ni wa Quraysh. Harb bin Umayyah (Baba yake mdogo Mtume (s.a.w)) ndiye alokuwa kiongozi wa vita kwa upande wa Mqauraysh na wasaidizi wake. Mwishoni mwa siku ya tano viongozi wa pande zote walikubali kuacha kupigana na wakaamuwa kufanya majadiliano ya amani kumaliza vita na hapa wakawekeana mkabata (maakubaliano) ulofahamika kwa jina la Al-Fudhul.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 669
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitabu cha Afya
HISTORIA YA NABII SHUAIB
Soma Zaidi...
Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo
i. Soma Zaidi...
Kisa cha Malkia wa Sabaa.
Sabaa ulikuwa mji katika nchi inayojulikana leo kama Yemen. Soma Zaidi...
tarekh
MAPIGANO YA AL-FIJAR (MAPIGANO YA UOVU). Soma Zaidi...
Hadhi na haki za Mwanamke katika jamii za Mashariki ya Kati bara la arabu hapo zamani
Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII MUSA(A.S) NA HARUN(A.S)
Nabii Musa(a. Soma Zaidi...
Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...
Vita vya Uhud na sababu ya kutokea kwake, Mafunzo ya Vita Vya Uhud
Vita vya Uhudi. Soma Zaidi...
Msonge wa uongozi na siasa katika serikali ya kiislamu mafinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
HISTORIA YA KUUMBWA KWA NABII ADAMU (A.S)NA HADHI YAKE NA HADHI YA WANAADAMU DUNIANI
Adam(a. Soma Zaidi...
TAREKH, HISTORIA NA SIRA YA UISLAMU NA MTUME MUHAMMAD KUTOKA KUZALIWA MPAKA KUFARIKI NA HARAKATI ZAKE
1. Soma Zaidi...