Kuzuka Imani ya Kishia
Baada ya kuuwawa Ali(r.a), kundi la marafiki wa Ali(Shi’a Ali) lilianzisha imani mpya ya ushia. Walifuata itikaqadi iliyo buniwa na ‘Abdallah bin Sabaa kuwa Ali ni Mrithi wa Mtume(s.a.w) kama Haruna(a.s) alivyokuwa mrithi Musa(a.s). Hivyo kundi hili liliitaqidi kuwa Ali(r.a) ndiye aliyekuwa Khalifa halali pekee na kuwaona Abubakar, ‘Umar na Uthmani kuwa walikuwa madhalimu waliopora nafasi hiyo. Siku zilivyosonga mbele mashia waliandika vitabu vyao vya sheria, Hadith, Historia ya Uislamu na ufafanuzi wa Qur’an unaolandana na imani yao mpya. Kwa mujibu wa Imani ya kishia, kiongozi wa jamii lazima aweImam ambaye uteuzi wakeunatokana na Mtume(s.a.w).
Baada yakut awafu Mtume(s.a.w),kulingana na Imani ya kishia Uimamu ulimshukia Ali(r.a) kupitia kwa mkewe Fatma bint Muhammed(s.a.w). Baada ya kuuliwa Ali(r.a) Uimamu uliwashukia watoto wa kiume wa Fatma hadi akafikia Imam wa kumi na moja anayeitwa Hassan al-Askari ambaye alifariki 874 A.D./260 A.H. katika utawala wa Abasi, ambao Khalifa wake alikuwa Matamid. Alipofariki Imam Hassan al- Askari Uimam ulimshukia mwanae Muhammad anayejulikana kwa jina la Mahdi, Imam wa mwisho.
Tarekh ya maimamu wa nyumba ya Mtume (Ahlul-Bayt) inatatanisha. Inaaminika Baba yake Hassan alihamishwa kutoka Madinah na kupelekwa Summara na dikteta Mutawakkil aliyekuwa Khalifa wakati huo, aliwekwa kizuizini huko Summara hadi akafa. Hassan naye aliwekwa kizuizini na aliyechukua nafasi ya Mutawakkil, mtoto wa Hassan aliyekaribia umri wa miaka mitano alianza kumtafuta baba yake katika pango lililokuwa karibu ya nyumba yao. Mtoto huyu hakurudi kutoka pangoni. Tukio hili limewapelekea Mashia kujaa matumaini kuwa mtoto huyu atarudi kuja kuikoa dunia kutokana na mzigo wa madhambi na uonevu.
Mtindo huu haumo katika mfumo wa Uislamu ingawa wafuasi wake wanatumia jina la Uislamu. Kwa nini mtindo huu haumo katika Uislamu tumeshazitaja sababu zake kuwa utume haurithiwi ila hapa tunataka kuongezea kuwa Imani hii ambayo ilipandikizwa baadaye katika historia ya Uislamu ina mizizi ya dini ya Uzoroastrian na Ukristu, dini ambazo zote zinamshirikisha Mwenyezi Mungu.
Angalizo(Tanbih)
Kwa Waislamu hivi leo, mfumo wa usia kama wanavyofanya wafuasi wanaojiita Mashia si katika utaratibu unaokubalika katika Uislamu. Mtume hakulifanya, na hata Ali alipokuwa katika kitanda cha mauti baada ya kujeruhiwa aliulizwa na mtu mmoja kuwa Waislamu wampe mkono wa ahadi ya utii mwanae mkubwa, Hassan, awe Khalifa? Ali alijibu, “Nawaachia Waislamu waamue”. Au mfumo wa ufalme (Royal Family) kama ule wa Saudia Arabia, Moroko, Oman, Qatar au mfumo wa vyama vingi au kimoja kama Pakistan, Misri, Libya, Syria n.k. siyo mifumo ya Kiislamu na nchi zinazofuata mifumo hiyo si za Kiislamu.
Hivyo ni dhahiri wajumbe wa Shura katika dola ya Kiislamu wanalazimika kwa kushirikiana na kiongozi aliyepo madarakani kumteua anayefaa kuwa kiongozi kisha jina liwasilishwe kwa waumini kwa ajili ya kupitishwa au kukataliwa. Hivyo ni kweli kuwa jina linalotolewa na utaratibu unaotumika sasa wa chama kuteua mgombea katika chaguzi za Marais duniani kote ni mawazo yaliyoazimwa kutoka katika mfumo huu wa Kiislamu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Mitume huzaliwa Mitume.
Soma Zaidi...Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w sehemu ya 18. Hapa utajifunza kuhusu tukio la kujengwa upya kwa al kaaba 🕋
Soma Zaidi...Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija.
Soma Zaidi...