Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani

Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani

Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani




VVU na UKIMWI ni mzigo mzito wa siri ambao watu wengi hawataki kutoa siri zao. Hii hupelekea kukaa muda mrefu akiwa na VVU ana UKIMWi bila hata kutumia dawa. Ni athari zipi anazipata. Hili hana haja nalo. Mwisho wa siku anafikia katika hatuwa ambao ni ngumu kurudi katika hali ya kawaida na hatimaye ni kifo.



Je unasubiliwa na mawazo kama umeathiria? Ni muda gani naweza kuishi na VVu na UKIMWI bila ya kupoteza maisha. Je ni zipi hasa dalili za kwanza kama una VVU na UKIMWI. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa tutakwenda kujibu maswali hayo na swali letu kuu lisemalo 'ni muda gani naweza kuishi na VVU na UKIMWI bila hata ya kutumia dawa za ARVs?



Dalili za VVU na UKIMWI huweza kujitokeza katika hatuwa kuu tatu. Katika hatuwa hizo tutaendelea kuona je ni muuda gani mtu anaendelea kuishi katika hali hizo bila ya kutumia dawa za ARV?



1.Katika hatuwa ya kwanza wiki ya 2 mpaka ya 4 baada ya kuathirika.
Hii ni hatuwa ya kwanza, punde baada ya kuathirika yaani kupata VVU. Hapa mwanzoni mtu atahidi dalili ambazo zinatokea wiki ya pili mpaka wiki ya nne. Kwa baadhi ya watu inaweza kufika mpaka wiki ya 6. katika kipindi hiki mgonjwa atona dalili kadha zitakazoonyeshwa hapo chini:-



Dalili za VVU ndani ya mwezi mmoja toka kuathirika
1.Homa
2.Maumivu ya viungo na misuli
3.Uchou
4.Kutokwa na jasho jingi usiku
5.Kutokwa na upele au ukurutu kwenye ngozi
6.Kutokwa na vidonda vya mdomo
7.Kuwashwa na koo ama vidonda vya koo
8.Kuvimba kwa tezi za limfu kwenye mapaja (mitoki) kwenye makwapa na kwenye shingo (tonsils)
9.Kichefuchefu na kutapika



Katika kipindi hiki virusi huendelea kuzaliana kwa kasi sana, na kujirundika kwa wingi sana kwenye damu kuliko maeneo mengine. Kipindi hiki huchukuwa wiki 2 mpaka nne ama 6 kwa wastani ni mwezi mmoja. Amam mmoja na nusu. Baada ya hapa mtu hatahisi dalili zingine za VVU wala UKIMWI. Katika kipindi hiki mtu anaweza kuambukiza wengine kwa urahisi.



2.Katika hatuwa ya pili kutoka kwezi mmoja na kuendelea.
Katika kipindi hiki virusi vinaanza kujichimbia ndani zaidi kwenye mwili. Uwingi wa virusi unasambaa maeneo mengine ya mwili na kuendelea kuambukiza wengine. Hatuwa hii mgonjwa kama hatatumia dawa za ARV anaweza kuishi mpaka miaka 10 ama zaidi ya hapo. Endapo mtu atatumia dawa virudi vitaweza kuzuiwakujizalia na hatimaye kupunguwa mwilini na vinawez akufikia katika hatuwa mabayo havionekani kabisa, ila mtu ataendelea kuwa muathirika, na ataendelea kutumia dawa.



Katika hatuwa hii hakuna dalili maalumu za VVU zitakazojitokeza. Yaani hakuna dalili yeyote katika hatuwa hii. Hatuwa hii ni mbaya sana kwani mtu anajihisi yupo sawa kiafya na hana shida yeyote, lakini virusi vinaendelea kuharibu kinga ya mwili kidogo kidogo. Mwishoni mwa hatuwa hii mtu atakuwa kinga yake imeshuka sana. Katika hatuwa hii mi bado haambiwi ana UKIMWI ila bado ni muathirika wa VVU



3.Hatuwa ya tatu, UKIMWI.
UKIMWI hutokea pale virusi vya VVU vinapoharibu kinga ya mtu hadi kufikia CD4 200. ipo hivi; mtu mwenye afya ya kawaida katika kila kipimo kimoja seli zake za CD$ zinakuwa kati ya 500 mpaka 1500. sasa endapo zitashuka na kufika 200 mtu huyu ataambiwa ana upungufu wa kinga mwilii yaani UKIMWI, tu endapo upungufu huu umesababishwa na VVU. Katika hatuwa hii kama mtu hatatumia dawa za ARV anaweza kuishi kwa miaka 3 baada ya hapo huwenda akafariki dunia.



Dalili za UKIMWI
1.Kutokwa na jasho jingi usiku
2.Homa za mara kwa mara
3.Kifua kikavu kisichopona
4.Maradhi ya ngozi na mdomo
5.Maambukizi na mashambukizi ya mara kwa mara
6.Kuharisha kusikokoma
7.Kupunguwa uzito



Kwa nini ni muhimu kutumia ARV?
Kwa kuwa sasa umeshajuwa kuwa usipotumia dawa unaweza kuishi zaidi ya miaka 10.sasa nikujuze faida za kutumia dawa hizi:-
1.Kuzuia uzalishaji wa virusi vya UKIMWi
2.Kuongeza umathubuti wa kinga ya mwili na kurefusha muda wa kuishi
3.Kupunguza uwezekano wa kuambukiza watu wengine.



Je naweza kufanya ngono na aliyeathirika na nisiathirike?
Ndio inawezekana kabisa kwa sababu zifuatazo:-
1.Kama umetumia kinga (kondomu)
2.Kama hakukutokea muchubuko wakati wa tendo la ndoa
3.Kama mgonjwa ametumia ARV kwa muda mrefu angalau kwa miezi 6 na kutumi na hali hiyo kwa muda zaidi hata akafikia kiasi idadi ya virusi haionekani kwenye kipimo.



Dawa ya kuzuia kuathirika kwa walio hatarini zaidi.
Kuna watu wapo hatarini sana kuathirika. Kwa mfano madaktari na wakunga, muda wowote wanaweza kuathirika. Shuikrani ziwaendee wataalamu wa dawa, wametuletea dawa inayotambulikwa kwa PrEP au kwa kirefu pre-exposure prophylaxis. Hii ji dawa inayotumika kwa dharura endapo umepatwa na mazingira hatarishi ambayo yanaweza kukupelekea kuathirika. Dawa hii inafanya kazi ndani ya masaa 72 baada ya kupata virusi. Tafiti zinaonyesha kuwa dawa hii ni bora kwa asilimia 80 inaweza kuzuia kmaambukizi ya muda mfupi.



Utaratibu wa maisha kwa aliyeathirika
1.Jilinde na maambukizi
2.Punguza misongo ya mawazo
3.Tumia kondomu wakati wa kushiriki ngono
4.Fanya mazoezi ya mara kwa mara
5.Kula mlo kamili
6.Wacha kuvuta sigara
7.Wacha ama punguza kutumia vilevi





                   



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 7128

Post zifazofanana:-

Fahamu vitamini C na kazi zake, vyakula vya vitamini C na athari za upungufu wake.
kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu. Soma Zaidi...

Makatazo ya kujiepusha nayo
Soma Zaidi...

KUWAHI KUMALIZA TENDO LA NDOA MAPEMA: kumwaga mbegu mapema
Hii ni hali inayowapata sana wanaume huwa wanamaliza hamu ya tendo la ndoa mapema kabla ya mwenza kuridhika. Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zabibu
Soma Zaidi...

Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Soma Zaidi...

Sababu za maumivu ya tumbo baada ya kula
Zijuwe sababu kuu za kuwepo kwa maumivu ya tumbo baada ya kula chakula Soma Zaidi...

SHIRK
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

Dalili za gonorrhea - gonoria
Jifunze dalili za gonorrhea na namna inavyoambukiza, zipi athari za gonori kwa wanawae na wanaume Soma Zaidi...

SIRI
Hapana mpaka sasa hautambui chochote kuhusu kilichotokea. Soma Zaidi...

MARADHI MENGINE 10 YANAYOTOKANA NA MBU ( matende, ngirimaji, homa ya manjano, n.k
Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende. Soma Zaidi...

NECTA FORM TWO MATHEMATICS (MATH) PAST PAPER
Soma Zaidi...

VITABU VYA AFYA
Soma Zaidi...