Ijuwe historia ya VVu, Dalili zake, tiba na vipimo vyake pia njia za kueneza VVU na UKIMWI
KUHUSU HIV NA UKIMWI
VVU ni kifupisho cha Virusi Vya Ukimwi. Kwa lugha ya kiingereza huitwa HIV kwa kurefusha ni Human immunodeficiency virus. Hivi ni virusi vinavyovunja na kuharibu uwezo wa mwili kujilinda dhidi ya maradhi na vijidudu vinavyoambukiza maradhi. Baada ya VVU kuingia mwilini na kuharibu kinga ya mwili, hupelekea kupata upungufu wa kinga mwilini ama hutwa UKIMWI.
Kuna aina kuu mbili za VVU navyo ni HIV-1 na HIV-2. aina ya kwanza ndiyo ambayo imeathiri watu wengi na ndio inayopelekea mgonjwa kupata madhara makubwa. Hii aina ya pili inapatikana Africa ya magharibi. Aina ya kwanza ndiyo ambayo imeenea karibia dunia nzima.
NINI CHANZO CHA VV NA UKIMWI?
Mpaka sasa chanzo halisi cha VVU bado ni mada tatizi. Ijap[okuwa wengi wanakubaliana na nadharia kuwa VVU asili yake ni masokwe, na ni huko Afrika huhusani maeneo ya Misitu ya Kongo. Yaani eti hapo zamani Waafrika wa maeneo hayo walikuwa wakiwinda masokwe kwa ajili ya kula nyama. Kumbe masokwe hayo yalikuwa na VVU. Hivyo kuingiliano huu ukapelekea watu kupata VVU. Kisha vikaanza kusafiri kutoka hapo, utandawazi na ukoloni, ukimbizi na miingiliano ya kibiahsara ilipelekea kuenea kwa kasi virusi hivi.
Kuna nadharia nyingine kuhusu chanzo cha VVu kama vile, inasemekean kuwa VVU ilitengenezwa maabara na wanasayansi wa marekani kwa ajili ya kupunguza wingi wa watu. Hii nadharia inakataliwa vikali kwani inapingana na historia pia inapingana na maeneleo ya sayansi na teknolojia.
Pia viongozi wa dini wanadhani kuwa VVU vililetwa na Mwenyezi Mungu kama ni Adhabu kwa wanadamu baada ya kuzidisha uovu, dhulma vitendo vingine vichfu. Hivyo Mungu akaleta gonjwa hili ili kuwaadhibu wanadamu.
Kwa ufupi zipo nadharia nyongi sana kuhusu chanzo na asili ya VVU. Hata hivyo wanasayansi wametokea kuikubali dhana ya kwanza kuwa VVU asili yake ni masokwe. Walipata kuchunguza na kugunduwa kuwa masokwenyanabeba virusi ambavyo vingeweza kuwa VVU baadaye baada ya michakato ya kigenetics.
DALILI ZA VVU
Dalilili za VVU huweza kutokea kuanzia wiki 2 mpaka 4 toka kuambukizwa. Lakini pia kwa baadhi ya ya watu inaweza kutokea mapema kabisa mnamo wiki ya kwanza. Na watu wengine dalili huizi zinaweza kutokea baadaye sana mpaka wiki ya sita. Dalili hizi si lazima mtu azipate zote. Dalili za mwanza zo VVU (HIV) ni pamoja na:-
Dalili za VVU katika hatuwa ya kwanza
1.Homa
2.Kuhisi baridi ama kutetemeka
3.Uota upele
4.Kutokwa na jasho wakatio wa usiku
5.Maumivu ya misuli
6.Kupata vidonda vya koo, ama kuwasha kwa koo.
7.Uchovu mkali usio elezeka
8.Kuvimba kwa tezi node za lymph yaani kuvimba tezi za mtoki mapajani, kwapa na shingoni.
9.Kupata vidonda kwenye mdomo
Dalili za VVU katika hatuwa ya pili
Baada ya dalili za awali katika hatuwa ya kwanza hadi kufikia wiki ya sita dalili za awali zitapotea. Kisha mtu ataingia katika hatuwa ya 2. hatuwa hii hujulikana kama clinical latency Stage ama pia huitwa chronic HIV infections. Hatuwa hii inaweza kuchukuwa mpaka miaka 10 toka kuambukizwa.
Watu waliokuwepo katika hatuwa hii hawana dalili yeyote ile. Kama mtu atatumia ART anaweza kudumu katika hatuwa hii kwa makumi ya miaka, ila kwa ambao hawajaanza kutumia ART wanaweza kupita kwa haraka kwenye hatuwa hii. Katika wakati huu mfumo wa kinga unaendelea kuharibiwa, ila uharibifu utakuwa mdogo ama hakuna endapo mtu ataanza kutumia ART au ARV.
HATUWA YA MWISHO NI UKIMWI
Ikitokea muathirika hakutimia ART basi virusi vitaendelea kuathiri mwili wake na kumaliza seli za CD4. hizi ndizo seli za kinga ya mwili yaani zinalinda mwili dhidi ya mashambulizi ya vijidudu kama virusi, bakteria, fangasi na vinginevyo. Mtu wa kawaida ana seli za cd4 kuanzia 500 mpaka 1500 katika kipimo kimoja. Sasa zikishuka mapaka kufikia 200 mgonjwa huyu ataambiwa ana Upungufu wa kinga Mwilini yaani UKIMWI. Mtu huyu atakuwa na dalili zifuatazo:-
Dalili za Ukiwmi:-
1.Kupunguwa uzito kwa haraka bila ya sababu maalumu ijulikanayo
2.Kupata homa kali za mara kwa mara na kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku.
3.Kuchovu mkali sana usiojulikana sababu.
4.Kuendelea kuvimba kwa tezi za mtoki, kwapa na shingo
5.Kuharisha kunakoendelea zaidi ya wiki moja
6.Kutokwa na vidonda kwenye mdomo, ulimi, mkundu na sehemu za siri.
7.Kubana kwa pumzi
8.Kupoteza kumbukumbu, kukasirika mara kwa mara, ama kupoteza uwezo wa kuthibiti akili (kuchanganyikiwa)
9.Kuota mapele, majipu, mabumbuza kwenye ngozi, kope, pua na mdomoni
VIPIMO VYA VVU:
VVU vinaweza kuonekana mapema sana kulingana na aina ya vipimo. Vipo vipimo ambavyo vinaweza kugunduwa virusi mapema sana hata ndani ya wiki. Hivi hutumiaka sana maabara na si rahisi kuvipata. Hapo chini nitataja baadhi ya vipimo ambavyo hupatikana karibia maeneo mengi
Kuna aina nyingi za vipimo vya VVU. Hapa nitataja baadhi tu ya aina za vipimo hivyo:-
1. Kipimo kinachohuisisha Muunganiko wa HIV antibody na antigen. Chenyewe kinaweza tu kupima damu ya mtu. Hivi vinatumika kugunduwa antigeni ijulikanayo kama p24. antigeni p24 ni chembechembe inayozalishwa mwilini baada ya kupata maambukizi, hivyo kama itakuwepo kwenye damu inamaana mtu atakuwa ameathirika. Kipimo hiki kinaweza kugunduwa virusi mwilini kuanzia wiki 2 mpaka 6 toka kuambukizwa. Yaani kuanzia wiki 2 mpaka mweni mmoja na nusu.
2.kipimo cha HIV antibody testing. Kipimo hiki kinaweza kupimwa kwa kuchukuwa damu ya mtu ama majimajinya wili wake. Chenyewe kinapima VVU mwilini kuanzia wiki ya 3 mpaka wiki ya 12 yaani wiki tatu mapaka miezi mitatu.
3.Kipimo kuangalia viral load; huu ni upimaji wa kiasi cha virusi kwenye kipimo cha damu. Ni kuwa kama kiasi cha virusi kwenye damu yako ni kikubwa sana unaweza kuwa dhaifu kuliko ambaye kiasi chake ni kidogo.
4.Kipimo cha kuangalia drugs resistance. Hapa ni kuangalia uwezo wa mwili kama utakuwa msugu kutumia aina flani ya ART.
MATIBABU YA VVU NA UKIMWI
Kama ijulikanavyo kuwa hakuna dawa ya kutibu kabisa IKIMWI ila zipo dawa za kusaidia kuishi nyema kama kawaida bila ya kupata usumbufu wowote. Dawa hizi husuia yharibifu wa mfumo wa kinga usiendelee. Kwa ufupi matibabu haya kuzuia ukuaji na uongezekaji wa VVU mwilini. Matibabu haya hujulikana kama ART. Yaani Anti Retroviral Theraphy, na dawa zake hujulikana kama ARV yaani Anti Retroviral Virus. Dawa hizi zimegawanyika katika makundi kama:-
1.Reverse transcriptase (RT) inhibitor. Hizi huzuia virusi kujizalisha na kuongezeka.
2.Protease inhibitors. Hufanya virusi vishindwe kufanya kazi vyema.
3.Fusion inhibitors. Hivi huzuia virusi kuingia mwilini
4.Integrase inhibitors. Hizi huzuia HIV kujizalisha
5.Multidrug combination. Huu ni muunganiko wa dawa hizi zaidi ya moja.
Namna ya kujikinga na VVU na UKIMWI
Watumiaji wa dawa hizi wanaweza kujihisi wapo salama, ila ukweli ni kuwa dawa hizi haritibu VVU hivyo wataendelea kuishi na VVU, na huku wanaendelea kupata tiba kwa uangalizi wa daktari.
Njia za kujikliga na VVU
1.Tumia kinga ya kondomu kila unapotaka kushiriki ngono
2.Hakikisha kama ni mjamzito unapata vipimo
3.Usishiriki sindano
4.Kuwa muaminifu kwa mwenza
Kushiriki ngono na mtu aliye na VVU na UKIMWI
Yes inawezekana, na hili ni swali watu wengi wamekuwa wakijiuliza. Itambulike kuwa kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika si lazima kuwa nawe utaathirika, ila kauli hii isieleweke vibaya. Kwani njia ambayo inaongoza leo katika kueneza maambukizi ya HIV ni kushiriki tendo la ndio. Mtu anaweza kushiriki tendo la ndoa na aliyeathirika bila ya kuathirika endapo:-
A.Endapo hakutatokea michubuko wakati wa tendo
B.Endapo muathirika ametumia dawa za ART kwa muda mrefu kwa kufuata masharti hata viral load yake ikawa haionekani (undetected) na akadumu kwa hali hii walau miezi 6
C.Endapo walitumia kinga wakati wa kushiriki tendo.
UNDETECTABLE VIRAL LOAD ni nini?
Kabla ya kujuwa maana nzima ya hii sentensi kwanza utambuwe maana ya viral load. Viral load ni idadi ya virusi vilivyomo kwenye damu katika kipimo. Sasa undetectavble viral load maana yake mtu ni muathirika ila virusi vyake idadi yake haionekani kwenye kipimo. Hapa anaweza kuwa pengine ana kirusi kimoja ama viwili ama hana kabisa. Itambulike kuwa hata kama virusi havionekani kwenye kipimo bado mtu atakuwa ni muathirika na kipimo cha ukimwi kitaendelea kumuonyesha ni muathiriki.a.
Muathirika aliyefikia hatuwa hii ataishi vyema kama watu wengine bila ya kuonyesha dalili yeyote ile. Pia kama ataendelea kudumu na hali hii kwa muda wa miezi kama 6 hatoweza kumuambukiza mtu kwa namna yeyote ile. Ma muathirika endapo atatumia vyema dawa za ARV anaweza kufikia kiwango hiki ndani ya mieze 6, ila kama atakuwa amechelea kuanza matibabu inaweza kuchukuwa muda zaidi ya hapo, na ndio maana watu wanashauriwa kupima ili kugunduwa maambukizi mapema iwezekanavyo.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Posti hii inazungumzia zaidi kuhusiana na Homa ya ini yenye sumu ni kuvimba kwa ini lako kutokana na kuguswa na vitu fulani ambavyo umeathiriwa navyo. Homa ya ini yenye sumu inaweza kusababishwa na pombe, kemikali, madawa ya kulevya au virutubisho vya lis
Soma Zaidi...Posti hii inaelezea kuhusiana na dalili za fangasi Mdomoni kwa watoto, vijana, watu wazima na mama wanaonyonyeshwa.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kutambua Dalili za macho makavu, kama tulivyotangulia kuona kubwa macho kuwa makavu Usababishwa na sehemu ya kuzalisha maji kwenye jicho kushindwa kufanya kazi na jicho hilo huwa kavu na Dalili zake ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Ma
Soma Zaidi...Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi.
Soma Zaidi...Makala hii itaeleza dalili za ukimwi, dalili za VVU, magonjwa nyemelezi na matumizi ya ARV
Soma Zaidi...HOMA YA DENGUEHoma ya dengue ni miongoni mwa maradhi hatari ambayo husambazwa na mbu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mkojo kushindwa kutoka kwenye kibofu na kwa kitaalamu huitwa retention of urine.
Soma Zaidi...Tetekuwanga (varisela) ni maambukizi ya virusi ambayo husababisha kuwasha, upele kama vile malengelenge. Tetekuwanga huambukiza sana watu ambao hawajapata ugonjwa huo wala kupewa chanjo dhidi yake. Kabla ya chanjo ya kawaida ya tetekuwanga, karibu watu
Soma Zaidi...