Maringo, majivuno, majigambo, dharau ni vipengele vya kibri. Kwa mujibu wa Hadith sahihi kibri ni katika madhambi makubwa"
"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ambaye moyoni mwake mna punje ya kibri hataingia peponi." Sahaba mmoja akauliza: "Je, kama mtu anapenda nguo nzuri na viatu?" Mtume (s. a.w) akasema, "Allah (s.w) ni mzuri na anapenda vizuri. Kibri ni kukataa ukweli na kupuuza watu." (Muslim)
Il i kuepukana na maringo na kibri Al l ah(s.w) anatutanabahisha:
"… Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa mlima." (1 7:3 7)
"Vipi mnamkanusha Mwenyezi Mungu na hali mlikuwa wafu, akakuhuisheni; kisha atakufisheni; kisha atakuhuisheni (tena); kisha kwake mtarejeshwa." (2:28)
Aliye bora mbele ya wengine ni yule aliyewazidi katika kumcha Mwenyezi Mungu - Rejea Qur-an (49:13)