Kujiepusha na kufuata mambo kwa kibubusa
Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki.
(g) Kujiepusha na kufuata mambo kwa kibubusa
Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki.
"Wala usifuate usiyo na ilimu (ujuzi) nayo. Hakika masikio na macho na moyo; hivyo vyote vitaulizwa." (17:36).
Kila mtu wa kawaida hana budi kutumia kipaji chake cha akili (moyo) na milango ya fahamu (macho, masikio, n.k.) katika kuchukua uamuzi sahihi na kufuata utaratibu wa maisha anaoridhia Allah (s.w). Na hasa kazi ya akili na kipaji cha elimu alichotunukiwa binaadamu, ni kumuwezesha kujitambua, kumtambua Mola wake na kumuabudu inavyostahiki.
Mtu atakayeishi kwa kufuata mambo kinyume na utaratibu anaoridhia Allah, ambao ni Uislamu, hatapaswa kumlaumu yeyote isipokuwa nafsi yake kwa matokeo mabaya yatakayomfika katika maisha ya dunia na akhera. Allah (s.w) anatutanabahisha juu ya hili katika aya zifuatazo:
(Wakumbushe wakati) waliofuatwa watakapowakataa wale waliowafuata, na hali ya kuwa wamekwisha kuiona adhabu, na yatakatika mafungamano yao. Na watasema wale waliofuata, "Laiti tungeweza kurudi (duniani) tukawakataa kama wanavyotukataa. "Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyowaonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni." (2:166-167)
Na wakasema wale waliokufuru: "Hat utaiamini Qur-an hii kabisa, wala Vile (vitabu) vilivyokuwa kabla yake." Na ungewaona madhalimu watakaposimamishwa mbele ya Mola wao, wakirudishiana maneno wao kwa wao, (ungeona mambo)! Wale wanyonge watawaambia wale waliojiona wakubwa: "Kama si nyinyi bila shaka tungekuwa Waislamu." Waseme wale waliojiona wakubwa kuwaambia wale wanyonge: "Oh!Sisi tulikuzuilieni uwongofu baada ya kukufikieni? (Siyo) Bali nyinyi wenyewe mlikuwa waovu. " Na wale wanyonge waseme kuwambia wale waliojiona wakubwa: "Bali (mlikuwa mkifanya), vitimbi (hila) usiku na mchana (vya kutuzuilia tusiamini); mlipotuamuru tumkufuru Mwenyezi Mungu na tumfanyie washirika." Nao wataficha majuto watakapoiona adhabu; na Tutaweka makongwa shingoni mwa wale waliokufuru; kwani wanalipwa mengine ila yale waliyokuwa wakiyatenda?" (34:31-33)
"Na (wakumbushe) watakapobishana katika Moto huo - wakati madhaifu watakapowaambia wale waliojitukuza: "Kwa yakini sisi tulikuwa wafuasi wenu, basi je, mnaweza kutuondolea sehemu kidogo ya Moto?" Waseme wale waliokuwa wakijitukuza: "Sisi sote tumo humu; Mwenyezi Mungu amekwishahukumu baina ya viumbe; (na tumekwishastahiki Moto, hatuna la kufanya." Na wale waliomo Motoni watawaambia walinzi wa Jahanamu; "Muombeni Mola wenu atupunguzie (alau) siku moja ya adhabu." (Walinzi) wawaambie: "Je, hawakuwa wakikujieni Mitume wenu kwa hoja zilizowazi?" Waseme: "Kwa nini? (Wakitujia lakini tuliasi)" Wawaambie: "Basi ombeni; na madua ya makafiri hayawi ila ni ya kupotea bure." (40:47-50)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 ai web app
Post zinazofanana:
Mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Ni upi mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu (EDK form 1: mgawanyo sahihi wa elimu kwa mtazamo wa uislamu
Soma Zaidi...Ni Ipi Elimu yenye manufaa
Elimu inaweza kugawanyika katika makundibmrngine mawili ambayo ni elimu yenye manufaa na elimubisiyi na manufaa
Soma Zaidi...Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Soma Zaidi...Nguzo za Imani kwa mujibu wa mafunzo ya kiislami.
Makala hii inakwenda kukufundisha kuhusu nguzo sita za imani katika Uislamu.
Soma Zaidi...NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.
Soma Zaidi...