Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.
Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.w) amelikataza si tu kulitenda, bali hata kulikurubia.
“Wala msikaribie zinaa. Hakika hiyo ni uchafu (mkubwa) na ni njia mbaya (kabisa) ". (1 7:32)
Watakao kiuka amri hii ya Allah (s.w), jamii ya Waislamu inalazimika kuwaadhibu wawili hao kwa adhabu iliyo sawa sawa kama inavyo bainishwa katika aya (24:2)
"Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mpigeni kila mmoja katika wao mijeledi (bakora) mia. Wala isiwashike kwa ajili yao huruma katika (kupitisha) hukumu hii ya Mwenyezi Mungu ikiwa nyinyi mnamuamini. Na lishuhudie adhabu yao (hii) kundi la waumini" (24:2)
Adhabu hii ni kwa wale ambao hawajaoa au hawajaolewa. Adhabu ya wazinifu ambao wameoa au kuolewa ni kurujumiwa (kupigwa kwa mawe) mpaka wafe kama tunavyojifunza katika Hadithi.
“Omar (r.a) amesimulia: "Hakika Allah (s.w) alimtuma Muhammad kwa haki, alimshushia kitabu (Qur'an). Katika aya alizoshusha Allah (s.w) palikuwa na aya ya kupiga mawe (wazinifu) mpaka wafe. Mtume wa Allah alihukumu kupigwa mawe (wazinifu) mpaka kufa na baada yake pia tuliwahukumu (Wazinifu) kupigwa mawe mpaka kufa. Na hukumu ya kupigwa mawe mpaka kufa katika kitabu cha Allah ni jambo la haki dhidi ya wanaume na wanawake waliozini wakiwa wameoa/wameolewa baada ya ushahidi kukamilika au baada ya kupata ujauzito au baada ya kukiri kufanya kitendo hicho" (Bukhari na Muslimu)
Jabir (r.a) ameeleza kuwa mtu alizini na mwanamke. Mtume (s.a.w) akapitisha hukumu dhidi yake na akachapwa viboko stahiki (100). Baadaye Mtume (s.a.w) alifahamishwa kuwa mtu yule alikuwa ameoa. Hivyo, Mtume (s.a.w) alipitisha hukumu stahiki dhidi yake na akapigwa mawe mpaka kufa" (Abu Daud)
Zinaa ni tendo la jimai lililofanywa baina ya mume na mke nje ya ndoa. Katika Uislamu na katika maadili mema ya kibinaadamu hapana ndoa inayokubalika baina ya jinsia moja, yaani ndoa ya mume kwa mume (ubasha) au mke kwa mke (usagaji). Pamoja na uovu wa zinaa, jimai baina ya jinsia moja, yaani Ubasha na Usagaji ni uovu uliokithiri. Watu waovu katika kaumu ya Nabii Lut (s.a) ikiwa ni pamoja na mkewe, waliangamizwa kutokana na kuzama kwao katika kutenda ovu hili.
“Na (wakumbushe) Luti alipowaambia watu wake: "Je, mnafanya uchafu, na hali mnaona?"
"Mnawaingilia wanaume kwa matamanio mabaya badala ya wanawake? Hakika nyinyi ni watu mfanyao ujinga kabisa." (27:54-55)
Pamoja na nasaha walizopewa na Mtume wao, Lut (a.s), watu hawa hawakutaka kubabili tabia yao chafu.
Basi haikuwa jawabu ya watu wake ila kusema: “Wafukuzeni wafuasi wa Luti katika mji wenu, hao ni watu wanaojitakasa, (basi wasikae na sisi wachafu)." (2 7:56)
Wakasema: “Kama usipoacha, ee Luti (kutukataza haya), bila shaka utakuwa miongoni mwa wanaofukuzwa (katika nchi hii)." (26:167)
Hukumu ya Allah (s.w) kwa watu hawa walionywa wasionyeke ilikuwa ni kuwaadhibu hapa hapa duniani na huko akhera wakiwa wanangojewa na adhabu kali.
Basi ilipofika amri yetu, tuliifanya ; juu yake kuwa chini yake, na tukawateremshia mvua ya changarawe za udongo mgumu (wa Motoni uliokamatana).
(Changarawe) zilizotiwa alama kwa Mola wako (kila moja kuwa ya mtu fulani). Na (adhabu) hii haiko mbali na madhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya). (11:82-83)
Mtume (s.a.w) amelikemea vikali na kulitolea hukumu ya kifo tendo la kaumu Lut (ubasha) kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:
Jabir (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Hakika jambo ovu la kutisha ninalokhofia umat wangu, ni tendo la kaumu Lut." (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah)
Akramah kutoka kwa Ibn Abbas (r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yeyote yule mtakayemshika kwa kosa la kufanya kitendo cha kaumu Lut, muueni yeye na yule aliyefanyiwa kitendo hicho." (Tirmidh, Ibn Majah)
Pamoja na ukubwa wa uovu wa matendo haya ya Ubasha na Usagaji, uliobainishwa wazi katika Qur'an na Hadith Sahihi za Mtume (s.a.w), leo hii duniani kuna nchi zilizo halalisha ndoa za jinsia moja na kutoa uhuru kamili wa kufanya matendo ya zinaa, ubasha na usagaji. Hiki ndio kiwango cha kuporomoka kwa maadili duniani hivi leo. Lakusikitisha zaidi, ni kwamba nchi zilizoporomoka kimaadili kiasi hicho, ndizo zinazojikweza kwa ustaarabu na uungwana na nchi nyingine zikiwemo za Waislamu kuzifanya viigizo.
Maovu haya ya uzinzi na ubasha yametolewa hukumu kali kiasi hicho cha kuchapwa mijeledi 100 mbele ya hadhara au kuuawa ili kuiokoa jamii ya binaadamu na madhara makubwa yanayosababishwa na maovu haya.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 919
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Kujiepusha na Kibri na Majivuno
Soma Zaidi...
Dalili (Alama) za Qiyama
Soma Zaidi...
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat al-Baqarah
Na katika watu, wako (wanafiki) wasemao: "Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho"; na hali ya kuwa wao si wenye kuamini. Soma Zaidi...
Mazingatio kabla ya kuosha maiti
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Hashir
Huwaoni wale wanafiki wanawaambia ndugu zao walio makafiri miongoni mwa watu waliopewa Kitabu (kabla yenu) Mayahudi (Wanawaambia): "Kama mkitolewa, (mkifukuzwa hapa) tutaondoka pamoja nanyi, wala hat utamtii yoyote kabisa juu yenu. Soma Zaidi...
Maadili katika surat luqman
Soma Zaidi...
Kwa namna gani Allah huwasiliana na wanadamu kwa kupitia ndoto.
Ndoto za kweli ni moja kati ya njia ambazo Allah huwasiliana na wanadamu. Soma Zaidi...
Sifa za waumini zilizotajwa katika surat Al-Anfal (8:2-4) na Al-Hujurat
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi. Soma Zaidi...
Dhana ya ibada kwa mtazamo wa uislamu..
Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Sifa za waumini wa ukweli katika uislamu
Je unamjuwq ni nani muumini, na ni zipi sifa za muumini? Soma Zaidi...
Nafasi ya Elimu katika uislamu
Elimu imepewa kipaumbele kikubwa kwenye uislamu. Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu nafasi ya Elimu katika uislamu. Soma Zaidi...
Muumini ni yule ambaye anazungumza ukweli
Ukweli ni katika sifa za waumini. Siku zote hakuna hasara katika kusema ukweli. Kinyume chake uongo ni katika madhambi makubwa sana. Soma Zaidi...