Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.
Kumzulia mtu mtwahirifu kuwa amefanya tendo la zinaa pasina kuleta ushahidi stahiki ni tendo ovu mno mbele ya Allah (s.w). Kina cha Uovu wa tendo hili la kuwasingizia uzinifu watu watwahirifu kinadhihirishwa na adhabu kali inayotolewa dhidi ya wazushi hawa:
“Na wale wanaowasingizia wanawake watahirifu (kuwa wamezini), kisha hawaleti mashahidi wanne, basi wapigeni mijeledi, (bakora) thamanini, na msiwakubalie ushahidi wao tena, na hao ndio mafasiki." (24:4)
"Bila shaka wale wanaowasingizia wanawake waliotakasika wasiojua (maovu), Waislamu; (wenye kuwasingizia watu hawa) wamelaaniwa katika dunia na akhera; nao watapata adhabu kubwa."
“Siku ambayo zitawashuhudia ndimi zao na mikono yao na miguu yao, kwa yale waliyokuwa wakiyafanya."
“Siku hiyo Mwenyezi Mungu Atawapa sawasawa malipo yao ya haki, na watajua kwamba Mwenyezi Mungu ndiye (Mwenye kulipa kwa) haki iliyo dhahiri."
(24:23-2 5)
Pia aya ifuatayo inakemea kwa ujumla juu ya tabia mbaya ya kuwasingizia (kuwazulia) watu wema kuwa wamefanya uovu, ili tu kuwadhalilisha na kuwaaibisha mbele ya jamii:
“Kwa yakini wale wannnaopenda uenee uovu kwa wale walioamini, watapata adhabu iumizayo katika dunia na akhera; na Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua; na nyinyi hamjui." (24:19)
Jambo la kuwasingizia uovu watu wema ni ovu mno mbele ya Allah (s.w) kwa sababu ndiyo silaha wanayotumia wanafiki na washirika wao katika kudhoofisha Uislamu kwa kuwakatisha tamaa wanaharakati na kuisambaratisha jamii ya Waislamu kwa ujumla. Katika historia ya Uislamu, wakati wa Mtume (s.a.w) silaha hii waliitumia wanafiki wakiongozwa na mkubwa wao Abdulllah bin Ubayy, walipomsingizia Bi Aisha (r.a), mkewe Mtume (s.a.w), kuwa amezini na Swafan bin Mu'attal Sulami, miongoni mwa maswahaba wema aliyeshiriki katika vita vya Badr. Allah (s.w) aliwatakasa waja wake hawa na uzushi wa wanafiki kwa kushusha Sura hii hasa katika aya zifuatazo:
Hakika wale walioleta uwongo huo (wa kumsingizia Bibi Aisha - mkewe Mtume -kuwa amezini) ni kundi miongoni mwenu, (ni jamaa zenu). Msifikiri ni shari kwenu, bali hiyo ni heri kwenu. Kila mtu katika wao atapata aliyoyachuma katika madhambi hayo. Na yule aliyejitwika sehemu yake kubwa miongoni mwao, atapata adhabu kubwa (zaidi)
Mbona mliposikia (habari) hii, wanaume Waislamu na wanawake Waislamu hawakuwadhania wenzao mema, na kusema "huu ni uzushi dhahiri?"
Mbona hawakuleta mashahidi wanne? Na walipokosa kuleta mashahidi, basi hao mbele ya Mwenyezi Mungu ni waongo.
Na kama isingalikuwa juu yenu fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema Yake katika dunia na akhera, bila shaka ingalikupateni adhabu kubwa kwa sababu ya yale mliyoyashughulikia.
Mlipoupokea (uwongo huo mkawa mnautangaza) kwa ndimi zenu na mkasema kwa vinywa vyenu msiyoyajua, na mlifikiri ni jambo dogo, kumbe mbele ya Mwenyezi Mungu ni kubwa. Na mbona, mliposikia, hamkusema: "Haitujazii kuzungumza haya: Utakatifu ni Wako (Mola wetu!) Huu ni uwongo mkubwa." Mwenyezi Mungu Anakunasihini msirudie kabisa kufanya mfano wa haya, ikiwa nyinyi ni Waislamu kweli. Na Mwenyezi Mungu anakubainishieni Aya (zake); na Mwenyezi Mungu ndiye Ajuaye, Mwenye hikima.' (24:11-1 8)
Kutokana na aya hizi tunajifunza yafuatayo:
(i) Waumini watakaposikia habari za uzushi dhidi ya watu wema,wasizikubali bali wadai ushahidi ulio wazi unaothibitisha tuhuma hizo.
(ii)Wazushi wakishindwa kuleta ushahidi, wachukuliwe moja kwa moja kuwa ni waongo na Waislamu wote wawe dhidi yao na kuwepo adhabu inayostahiki.
(iii)Ni marufuku kwa waumini kudaka na kutangaza mambo ya uzushi dhidi ya watu wema ambayo hawana hakika nayo. Katika kusisitiza hili Allah anatuasa:
“Enyi mlioamini! Kama fasiki, (asiyekuwa wa kutegemewa) akikujieni na habari (yoyote ile msimkubalie tu) bali pelelezeni (kwanza), msije mkawadhuru watu kwa ujahili na mkawa wenye kujuta juu ya yale mliyoyatenda. ”(49:6)
(iv)Waislamu wanahimizwa wajenge tabia ya kuwa na dhana njema juu ya waumini wenzao kuwa haiwezekani kwa muumini kufanya tendo hilo chafu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 345
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 kitabu cha Simulizi
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Simulizi za Hadithi Audio
👉5 Madrasa kiganjani
👉6 Kitau cha Fiqh
Imani ya Kiislamu na ni nani muumini?
Soma Zaidi...
Kwa nini Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kufuatwa
Kwa nini uislamu ndio dini pekee ya haki ambayo watu wanatakiwa waifuate. Soma Zaidi...
Humtegemea Mwenyezi Mungu peke yake
Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu. Soma Zaidi...
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo
Mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na nini?
(EDK form 1: mgawanyo wa elimu usiokubalika katika uislamu unasababishwa na sababu zifuatazo) Soma Zaidi...
UMBILE LA MBINGU NA ARDHI
“Katika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s. Soma Zaidi...
Mgawanyiko wa Elimu kwa mtazamo wa kikafiri
Kwa mtazamo wa kikafiri elimu imegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Elimu ya dunia na Elimu ya akhera. Soma Zaidi...
Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kumuamini mwenyezi Mungu (S.W)
Nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...
Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...
Kutopupia dunia
"Ewe mwanangu! Soma Zaidi...
Himizo la kuwasamehe waliotukosea
“Na wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita). Soma Zaidi...