image

vigawanyo vya elimu

Katika Uislamu Hakuna Elimu ya Dini na Dunia



Makafiri na hata baadhi ya Waislamu kutokana na mtazamo wao finyu juu ya maana ya dini iliyowapelekea kuyagawanya maisha ya binaadamu kwenye matapo mawili; maisha ya dini na maisha ya dunia, wameigawanya elimu kwenye matapo hayo mawili.


Kwa mtazamo huu potofu elimu ya dini ni ile inayoshughulikia maswala ya kiroho (spiritual life) ya mtu binafsi inayoishia katika kumuwezesha mtu kuswali, kufunga na kutekeleza Ibada nyingine maalumu kama hizi bila ya kuzihusisha na maisha yake ya kila siku ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.


Hivyo elimu hii haina nafasi ya kumuwezesha binaadamu kuendea maisha yake ya kila siku ya kijamii.



Elimu ya Dunia kwa mtazamo huu wa makafiri, ni ile inayojishughulisha na masuala ya kijamii kama vile uchumi, siasa, utamaduni, sheria na maongozi ya jamii kwa ujumla kwa kufuata maelekezo na matashi ya binaadamu bila ya kuzingatia mwongozo wa Allah (s.w).



Kwa mtazamo wa mgawanyo huu, elimu ya dini ndiyo iliyofundishwa na Allah (s.w) kupitia kwa Mitume na Vitabu vyake na elimu ya dunia imebuniwa na binaadamu wenyewe kwa msukumo wa matashi na mahitaji yao katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kimaada (Physical or Material life)


.
Kwa mtazamo wa Uislamu (Qur-an na Sunnah) hapana mgawanyo huu wa elimu kwa sababu za msingi zifuatazo:
Kwanza, Nabii Adam (a.s) katika kuandaliwa yeye na kikazi chake kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni alifundishwa majina ya vitu vyote kama Qur-an inavyoainisha:



“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha Adam majina ya vitu vyote…” (2:31).
Majina ya vitu vyote hapa kama tulivyotangulia kusema inaashiria fani zote za elimu zitakazomuwezesha binaadamu kuendea kila kipengele cha maisha yake na kufikia malengo tarajiwa.


Pamoja na kufundishwa majina ya vitu vyote, pia Adam (a.s) na kizazi chake waliahidiwa na Mola wao kuletewa mwongozo utakaowawezesha kutumia fani mbali mbali za taaluma walizonazo kwa kufuata utaratibu utakaowapelekea kukiendea kila kipengele cha maisha yao kwa furaha na amani:
“Tukasema: Shukeni humo nyote; na kama ukikufikieni uwongozi utokao kwangu, basi watakaofuata uwongozi wangu huo, haitakuwa khofu juu yao wala hawatahuzunika.” (2:38).



Lakini wale watakaotumia taaluma mbali mbali walizonazo katika kuendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii bila ya kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mitume wake na Vitabu vyake, wataishi maisha ya huzuni na khofu na katika maisha ya akhera watakuwa na adhabu kali:
“Lakini wenye kukufuru na kuyakadhibisha maneno yetu, hao ndio watakaokuwa watu wa motoni, humo watakaa milele.” (2:39)


Kwa mujibu wa maelezo haya tunajifunza kuwa fani zote za elimu (majina ya vitu vyote) ambazo amezifundisha Allah (s.w) pamoja na mwongozo maalumu kutoka kwake, vinahitajika kwa binaadamu ili kumuwezesha kuishi maisha ya furaha na amani hapa duniani na huko akhera.


Hivyo hapana mwenye uwezo wa kutenganisha maisha ya dini na dunia au elimu ya dini na dunia.
Pili, Amri ya kusoma (kutafuta elimu) aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake, haibagui elimu ya dini na dunia.


Vinginevyo fani yoyote ya elimu inayomuwezesha binaadamu kusimamisha ukhalifa wa Allah (s.w) katika jamii na kufikia lengo la kuumbwa la kumuabudu Allah (s.w) inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake inapaswa isomwe kwa juhudi zote.



Tatu, chanzo cha fani zote za elimu ni Allah (s.w) kama Qur-an inavyosisitiza:


“Soma na Mola wako ni karimu sana. Ambaye amemfundisha (Binaadamu fani zote za elimu) kwa msaada wa kalamu. Amemfundisha mwanaadamu (chungu ya mambo) aliyokuwa hayajui”. (96:3-5)
Kwa mujibu wa aya hizi hapana fani yoyote ya taaluma iliyoasisiwa na binaadamu. Hivyo suala la kuwa na elimu ya dunia iliyoasisiwa na binaadamu na elimu ya dini ambayo tu ndiyo iliyotaka kwa Allah (s.w), halipo kwa mtazamo wa Qur-an.



Nne, katika Qur-an tunafahamishwa kuwa wanaomcha Allah (s.w) ipasavyo na kumuogopa ni wale wataalamu (ulamaa) waliozama katika fani mbali mbali za elimu. Kwa mujibu wa Qur’an fani hizi mbali mbali haziishii tu kwenye zile fani zinazotazamwa kwa mrengo wa kidini kama vile fiqh, Tawhiid, n.k. bali fani zote za elimu zinazo muwezesha binaadamu kutafakari kwa undani juu ya kuwepo Allah (s.w) na daraja ya utukufu wake, hasa zile fani za kisayansi zinazohusiana na maumbile. Hebu turejee aya zifu atazo:



Je! Huoni kwamba Mwenyezi Mungu ameteremsha maji toka mawinguni! Na kwayo tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana. (35:27)


Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali. Kwa hakika wanaomwogopa Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanavyuoni). Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Msamehevu.


(35:28)
Katika aya hizi tunajifunza kuwa wenye kumcha Allah (s.w) ipasavyo na katika kiwango cha juu cha unyenyekevu ni wale waumini waliobobea katika taaluma mbali mbali (maulamaa).


Je, maulamaa waliotajwa katika aya hizi ni wale tu waliobobea kwenye taaluma zinazoitwa za kidini kama vile fiq-h, Qur-an na Hadith? Maulamaa waliopigiwa mfano katika aya hizi ni wale waliozama katika fani ya Hali ya Hewa (Meteorologist), Maulama waliozama katika uchunguzi wa wanyama (Zoologist), maulamaa waliozama katika fani ya matunda (Horticulturist), Maulamaa waliozama katika fani ya Madini (Geologists) na Maulamaa waliozama katika fani ya kuchunguza watu walivyo kimaumbile, rangi, n.k. (Anthropolagist).


Pia katika aya nyingi za Qur-an binaadamu


amesisitizwa kuyafanyia utafiti mazingira ya mbingu na ardhi ili kumtambua Mola wake na kumuabudu ipasavyo.
Tano, katika Qur-an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini waliobobea kwenye elimu wana daraja kubwa zaidi kuliko waumini wengine:


“… Mwenyezi Mungu atawainua wale walioamini miongoni mwenu; na waliopewa elimu watapata daraja zaidi. Na Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda yote.” (58:11)
Aya hii haijabagua wenye elimu.


Hivyo yeyote yule mwenye taaluma inayomuwezesha kumcha Mola wake na kumuabudu inavyostahiki katika kila kipengele cha maisha yake na ikamuwezesha kuchangia katika kusimamsiha Uislamu katika jamii atakuwa na daraja zaidi kuliko wale wasio na taaluma hiyo kama Qur-an inavyozidi kusisitiza:


“… Hakika ahishimiw aye sana miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mw enyezi Mungu zaidi katika nyinyi.” (49:13)
Sita, hatuoni mgawanyo wa elimu katika Hadith mbali mbali za Mtume (s.a.w) zinazozungumzia elimu. Kwa mfano Mtume (s.a.w) aliposema: “Kutafuta elimu ni faradhi kwa kila Muislamu mwanamume na kila Mu is lamu mwanamke.


” (Ibn Majah), hakubagua elimu. Pia rejea Hadith zifuatazo:
Anas (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema: Mw enye kutoka nje kutafuta elimu yuko katika njia ya Allah mpaka atakapo rejea. (Tirmidh).


Abu Hurairah (r.a) ameeleza kuwa Mtume (s.a.w) amesema:Yeyote atakayeulizwa juu ya jambo alilojifunza kisha akaficha (akakataa kutoa elimu ile) atavalishwa mshipi (mkanda) wa Moto siku ya Kiyama.” (Ahmad, Abu Daud, Tirmidh na Ibn Majah).



Pia tunajifunza katika historia kuwa Mtume (s.a.w) aliwaacha huru mateka wa vita vya Badr kwa yule aliyeweza kujikomboa kwa kuwafunza kusoma na kuandika watoto kumi wa Waislamu.


Hadith hizi zinadhihirisha kuwa Mtume (s.a.w) naye hakuigawanya elimu katika elimu ya dini na elimu ya dunia. Bali Mtume (s.a.w) amewahimiza Waislamu kutafuta elimu yenye manufaa kwa jamii popote pale inapopatikana.



“Tafuteni elimu hata China” (Baihaqi).
Laiti kama pangelikuwepo na mgawanyo wa elimu na kuwa elimu ya lazima kutafutwa na Waislamu ni ile iitwayo “elimu ya dini” kwanini Mtume (s.a.w) aliwaamuru waende China wakati wahay ulikuwa unamfuata yeye alipo? Ilikuwa inatosha wao kubaki na Mtume Makkah au Madina na asiwatume tena kwenda China kutafuta elimu.



Hivyo, kutokana na hoja hizi sita, Uislamu hautambui mgawanyo wa elimu kwenye tapo la elimu ya dini na elimu ya dunia.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 271


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 kitabu cha Simulizi     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Sifa na majina ya siku ya mwisho siku ya kiyama
Soma Zaidi...

mgawanyiko wa elimu
Soma Zaidi...

Mgawanyo wa Elimu Usiokubalika katika uislamu.
Kipengele hichi kinahusu mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu.sababu za mgawanyiko wa elimu udio sahihi katika uislamu. Soma Zaidi...

Haki za kielimu za mwanamke katika uislamu
Haki ya ElimuKatika Uislamu kujielimisha ni faradhi inayowahusu Waislamu wote, wanaume na wanawake: "Soma kwa jina ? Soma Zaidi...

Mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na maumbile yake
Kuwa ni kwa nini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini kutokana na umbile la mwanadamu. Soma Zaidi...

Historia ya Mwanadamu
Soma Zaidi...

Kuamini siku ya mwisho
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu Soma Zaidi...

Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu Soma Zaidi...

Nguzo za imani
Zifuatazo ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya dini ya kiislamu) Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMANI
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s. Soma Zaidi...

Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?
Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kwa nini hakuna haja ya Mtume mwingine baada ya Muhammad
Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an. Soma Zaidi...