1.
1.Dhikri ya kuleta wakati wa kuamka kutoka usingizini Mtume (s.a.w) alipoamka kutoka usingizini alikuwa akisema: Al-hamdulillahilladhy ahyaanaa ba'adamaa amaatanaa wailayhi nnushuuru" โSifa zote njema anastahiki Allah ambaye ametupa uhai baada ya kutufisha na ni kwake tu ufufuo." Mtume (s.a.w) amesema: "atakaye amka usiku kisha akasema: Laailahaillallaahu wah-dahu laa shariika lahu, lahulmulku walahul-hamdu wahuwa a'laa kulli shay-in qadiiru, โHapana Mola ila Allah, Mpweke asiye na mshirika, ni wake ufalme na ni zake sifa njema, ni muweza juu ya kila kitu; Kisha akasema "Rabbigh-fir-ly" โEe, Mola nisamehe" Basi atasamehewa. Na kama atasimama akaenda kutawadha kisha akaswali basi swala yake itakubaliwa."
2.Dhikri ya kuleta wakati wa kuvaa nguo Al-hamdulillaahi lladhy kasaany hadha (thawba) warazaqaniihi min ghairi hawlin minny walaaquwwat" "Sifa zote njema ni za Allah ambaye amenivisha nguo hii na kuniruzuku pasina uwezo wala nguvu kutoka kwangu."
3.Dua ya Kuvua Nguo "Bismillah" "Kwa jina la Allah (nina vua)."
4.Dua ya Kuingilia Chooni Muislamu akiingia chooni atangulize mguu wa kushoto na kusema: (Bismillah) โAllahumma inni a'uudhubika minal-khubuth wal-khabaaithi" (Kwa jina na Allah). Ee, Allah najikinga kwako na maovu yote na wafanya maovu"
5.Dua ya Kutoka Chooni Muislamu akitoka chooni hutanguliza mguu wa kulia na kusema: โGhuf-raanaka" โNakuomba msamaha (Ee Allah)
6.Dhikri wakati wa kutoka Nyumbani Bismillahi tawakkal-tu 'alallaahi walaahawla walaaquwwata illaabillaahi Kwa jina la Allah, ninajitegemeza kwa Allah, na hapana uwezo wala nguvu ila vyote vinatokana na Allah"
7.Dhikri wakati wa kurejea nyumbani Bismillahi walaj-naa, wabismillaah kharaj-naa wa'alaa Rabanaa tawakkal-naa. โKwa jina la Allah tunaingia na kwa jina la Allah tunatoka, na kwa Mola wetu tunategemea."
8.8.Dua ya Kuingia Msikitini Tukiingia msikitini tunatanguliza mguu wa kulia na kusema: โA'udhubillaahil-'adhiim wabiwajhi-hil-kariim. 'Wasul-Twaanihil-qadiimi minash-shaytwaanir rajiim Bismillaah wasw-swallatu wassalaam aโlaa rasuulillah , Allaahummaf-tahaly ab-waaba rah-matika". โNajikinga kwa Allah aliye mtukufu, na kwa uso wake mtukufu, na kwa utawala wake wa kale, kutokana na sheitwani aliyeepushwa na rehema za Allah,Kwa jina la Allah na Rehma na Amani ziwafikie Mtume wa Allah Ee! Allah nifungulie milango ya rehema zako."
9.9.Dua ya kutoka Msikitini Tukitoka msikitini tunatanguliza mguu wa kushoto na kusema: โBismillahir wasw-swalaatu was-salaamu 'alaa rasuulillaahi, Allaahumma inny as-aluka min fadh-lika, Allaahumma A'iswimniy, minash-shaytwaanir-rajiimi." โKwa jina la Allah na rehema na amani zimfikie Mtume wa Allah; Ee! Allah,nakuomba katika fadhila zako, Ee! Allah nilinde kutokana na shetani aliyeepushwa na rehema zako (aliye laaniwa)."
10.Dhikri za Kuleta Asubuhi na Jioni โAllahumma 'aafiniy fiy badaniy,Allahumma 'aafiniy fiy sam-'iy. Allahumma 'aafiniy fiy baswariy,Laailaha illaa anta. (Mara tatu) Ee! Allah nipe afya ya mwili wangu,Ee! Allah nipe afya ya usikivu wangu (masikio yangu),Ee! Allah nipe afya ya uoni wangu (macho yangu). Hapana Mola ila wewe (mara tatu).
Umeionaje Makala hii.. ?
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa.
Soma Zaidi...Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Ninichanzo cha Elimu? (EDK form 1 Dhanaya Elimu)
Soma Zaidi...Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุฑูููุฑูุฉู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ู ููู ููุงูู ููุคูู ููู ุจูุงููููููู ููุงููููููู ู...
Soma Zaidi...ุนููู ุนูู ูุฑู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุฃูููุถูุง ููุงูู: " ุจูููููู ูุง ููุญููู ุฌููููุณู ุนูููุฏู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ุฐูุงุชู ููููู ูุ ุฅุฐู ?...
Soma Zaidi...Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...