Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:1 Kumuamini Allah (s.
Tunajifunza katika Qur-an na hadithi sahihi kuwa Imani ya Kiislamu imejengwa juu ya nguzo sita zifuatazo:
1 Kumuamini Allah (s.w).
2 Kuamini Malaika wake.
3 Kuamini Vitabu vyake.
4 Kuamini Mitume wake.
5 Kuamini Siku ya mwisho.
6 Kuamini Qadar yake.
Hawi Muumini wa Kiislam yule ambaye amekanusha angalau moja ya nguzo hizi kama inavyobainika katika Qur-an:
“... Na mwenye kumkanusha Allah (s.w) na Ma la ika wake na Vitabu vyake na Mitume wake na siku ya mwisho., basi bila shaka amepotea upotofu ulio mbali (kabisa)” (4:136)Mtu hatakuwa Muumini kwa kutamka tu hizi nguzo sita, bali pale atakapozijua kwa undani na kuendesha maisha yake yote kwa misingi ya nguzo hizi.
Tunazifahamu nguzo hizi sita kutokana na Hadith ya Mtume (s.a.w) iliyosimuliwa na Umar (r.a) kama ifuatavyo:Siku moja tulipokuwa tumeketi pamoja na Mtume (s.aw.) alitutokea mtu mmoja ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe kama theluji na nywele zake nyeusi sana, hakuwa na dalili zozote za msafiri, ingawa alikuwa mgeni kwetu sote.
Halafu alikaa mbele ya Mtume (s.a.w) hali magoti yake yakikabiliana na yale ya Mtume na akaweka mikono yake katika mapaja ya Mtume na akasema:”Ewe Muhammad nifahamishe juu ya Uislamu ” na Mtume akasema ; “Ni kushuhudia ya kuwa hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah, Kusimamisha swalaa, kutoa Zakat, Kufunga Mwezi wa Ramadhani, Kuhiji Makkat kwa mwenye kuweza” Halafu yule mgeni akasema “umesema kweli”. Tukastaajabu kwa nini aliuliza halafu akasadikisha.
Halafu akasema; “Nifa ham ishe juu ya Iman ”. Mtume akasema : “Ni kumuamini Mwenyezimungu na, Ma la ika wake , Vitabu vyake, Mitume wake, Siku ya Mwisho na Qadar, Kheri na shari yake.
Kisha akasema nifahamishe juu ya Ihsaan” Akasema “Ni Kumuabudu Allah kama kwamba unamuona, ikiwa wewe humuoni yeye anakuona ” Halafu akasema nifahamishe juu ya Kiyama ” Akasema: “Hajui mwenye kuulizwa juu ya hilo zaidi ya mwenye kuuliza.
Akasema “Nifahamishe dalili zake. Mtume akasema: “Ni wakati ambapo mjakazi atamzaa bibi yake, na utakapowaona wachungaji masikini wanaposhindana kujenga maghorofa. “Yule mgeni alipoondoka, Mtume alikaa kimya kwa muda kisha akasema: “eweUmar, unamfahamu muulizaji?’ Sote tukamjibu kuwa Allah na Mtume wake wanajua zaidi. Mtume akasema “Huyo ni Jibriil amekuja kuwafundisheni dini yenu” (MUSLIM)
Umeionaje Makala hii.. ?
"Hakika wanaoamini kweli ni wale ambao anapotajwa Allah nyoyo zao hujaa khofu; na wanaposomewa aya zake huwazidishia imani na wanamtegemea Mola wao tu basi.
Soma Zaidi...Somo Hili linaeleza kuhusu mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.
Soma Zaidi...Waislamu wanakatazwa kufanya na kufuata mambo kwa kibubusa (kwa mkumbo) bila ya kuwa na ujuzi unaostahiki.
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.
Soma Zaidi...Mtu hawi Muumini wa kweli mpaka awe na yakini juu ya vitabu vya Allah (s.
Soma Zaidi...