Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).
Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu ni:
Il-hamu.
- Ni mtiririko wa habari (ujumbe) unaomjia mwanaadamu bila kufundishwa na mtu yeyote au kuona mfano wake katika mazingira yeyote.
Kuongea na Mwenyezi Mungu (s.w) nyuma ya pazia.
- Ni njia mwanaadamu huongeleshwa na Mwenyezi Mungu (s.w) moja kwa moja kwa sauti ya kawaida bila kumuona.
- Nabii Musa (a.s) ni miongoni mwa Mitume waliosemeshwa na Allah (s.w) nyuma ya pazia.
Rejea Qur’an (28:30), (7:143) na (19:23-26).
Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa.
- Ni njia anayoitumia Allah (s.w) kumuelimisha mwanaadamu kwa kupeleka ujumbe kupitia mitume na watu wengine wema.
Rejea Qur’an (53:1-12), (15:51-66), (19:16-19), (2:102) na (3:41).
Ndoto za kweli (ndoto za mitume).
- Ni kupata ujumbe kupitia ndoto za kweli hasa kwa mitume ambayo huwa ni maagizo ya Allah (s.w) kwa Mitume.
- Mfano ndoto ya Nabii Ibrahim (a.s) juu ya kumchinja mwanae Nabii Ismail (a.s).
Rejea Qur’an (37:102), (12:4-5), (12:100) na (48:27).
Njia ya Maandishi (mbao zilizoandikwa).
- Ni njia ya mawasiliano ya Allah (s.w) na waja wake kupitia maandishi yaliyoandikwa tayari.
- Nabii Musa aliletewa ujumbe kwa maandishi kutoka kwa Allah (s.w).
Rejea Qur’an (7:145) na (7:154).
Umeionaje Makala hii.. ?
Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu
Soma Zaidi...Hawamuogopi au kumtegemea yeyote kinyume na Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu juu ya ibada (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.
Soma Zaidi...