Kujiepusha na Kibri na Majivuno
(h) Kujiepusha na Kibri na Majivuno
"Wala usiwatizame watu kwa upande mmoja wa uso (usiwafanyie watu jeuri) Wala usiende katika nchi kwa maringo; Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunaye, ajifaharishaye" (31:18)
"Wala usitembee (usiende) katika ardhi kwa maringo. Hakika wewe huwezi kuipasua ardhi wala huwezi kufikia urefu wa mlima. Haya yote ubaya wake ni wenye kuchukiza mbele ya Mola wako" (17:37-38)
Kibri ni tabia ya kukataa ukweli na kuwadharau watu kama tu navyoj ifu nza katika Hadithi ifuatayo:
"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa, Mtume wa Allah am esem a, "Yule ambaye moyoni mwake mnachembe ya kibri hataingia peponi" Swahaba mmoja akauliza: "Je kama mtu anapenda nguo nzuri na viatu?" Mtume (s. a.w) akasema, "Allah (s.w) ni mzuri na anapenda vizuri. Kibri ni kukataa ukweli na kupuuza watu ". (Muslimu)
Vile vile kibri na majivuno ni tabia ya kishirikina kama tunavyojifunza katika Hadithi nyingine ifuatayo:
"Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema; Allah akasema; Utukufu ni nguo yangu na kibri ni kilemba changu. Yeyote atakaye shindania kimoja wapo katika hivi ataangamia." (Muslimu)
Mtu mwenye kibri na majivuno daima atakuwa ni mpinzani wa harakati za kusimamisha Uislamu katika ardhi, kwani atapendelea utawala ule ambao utamfanya kuwa mungu katika jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Bongolite - Game zone - Play free game π2 web hosting π3 Dua za Mitume na Manabii π4 ai web app π5 Simulizi za Hadithi Audio π6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina
Post zinazofanana:
Mgawanyiko wa elimu usiokubalika katika uislamu
Ni mgawanyo upi wa elimu haukubaliki. Ni ipi elimul akhera na elimu dunia? (Edk form 1 Dhana ya elimu)
Soma Zaidi...Maana ya kuamini malaika katika maisha ya kila siku
Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Himizo la kuwasamehe waliotukosea
βNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...Sifa za Waumini zilizotajwa katika surat Ahzab
Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa
Soma Zaidi...