KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU

KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU


KUMUAMINI MWENYEZIMUNGU


Nafasi ya akili katika kumtambua Allah (s.w)



Imani ya kweli juu ya Allah (s.w) itathibitika moyoni baada ya kumjua vyema Allah (s.w) na sifa zake zote tukufu. Allah (s.w) hatumuoni kwa macho bali tunamfahamu kwa akili zetu katika kuchunguza dalili mbali mbali zilizotuzunguka.


Tunavyojifunza katika Qur-an, matumizi ya kwanza ya akili tulizotunukiwa ni kuyakinisha kuwepo kwa Allah (s.w) na sifa zake. Msisitizo wa matumizi ya akili na fikra zetu katika kazi hii ya kumjua Allah (s.w) na sifa zake tukufu unabainishwa katika aya zifuatazo:โ€œKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana ziko hoja (za kuonyesha kuwepo Mwenyezi Mungu - Allah) kwa wenye akiliโ€. (3:190).


โ€œNa katika ishara zake, (za kuthibitisha kuwepo kwake na uweza wake) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kutoka kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofa hamuโ€ (30:21)



โ€œNa katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuziโ€. (30:22).


โ€œNa katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.โ€ (30:23)


โ€œNa katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamuโ€ (30:24)
Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo:



โ€œJe! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(35:27)


Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.โ€ (35:28)
Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za โ€œdiniโ€ bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an:



โ€œNa bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79)


โ€œHakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)โ€ (8:22).


Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu.


Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20)


Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8).
Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni:
Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake
Nafsi ya mwanaadamu
Historia ya mwanaadamu
Maisha ya Mitume
Mafundisho ya Mitume


โ€œNa katika ishara zake (za kuonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi na kuhitalifiana lugha zenu na rangi zenu na (mengine yenu na hali ya kuwa muumbaji ndiye huyo huyo mmoja). Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuziโ€. (30:22). โ€œNa katika ishara zake ni kulala kwenu usiku na (kuamka) mchana, na kutafuta kwenu fadhila yake. Hakika katika hayo zimo ishara kwa watu wanaosikia.โ€ (30:23) โ€œNa katika ishara zake ni kukuonyesheni umeme kwa (kukutieni) hofu na tamaa (ya kuja mvua), na kuyateremsha (hayo) maji kutoka mawinguni. Kwayo huifufua ardhi baada ya kufa kwake. Bila shaka katika haya zimo ishara kwa watu wanaofahamuโ€ (30:24) Aya hizi chache zatosha kuonesha msisitizo wa Qur-an juu ya kutumia akili na fikara zetu katika kumfahamu vyema Allah (s.w). Kila mtu atakavyozama katika utafiti wa mazingira katika fani yoyote ile ndivyo atakavyoweza kumuona Allah (s.w) na utukufu wake kwa upeo mkubwa zaidi. Allah (s.w) mwenyewe anathibitisha hilo katika aya zifuatazo: โ€œJe! Huoni kwamba Mw enyezi Mungu Ameteremsha maji mawinguni! Na kw ayo Tumeyatoa matunda yenye rangi mbali mbali. Na katika milima imo mistari myeupe na myekundu yenye rangi mbali mbali, na (mengine) myeusi sana.(35:27) Na katika watu na wanyama wanaotambaa na wanyama (wengine), pia rangi zao ni mbali mbali, kwa hakika wanaomcha Allah miongoni mwa waja Wake ni wale wataalamu (wanazuoni): Bila shaka Mwenyezi Mungu ni Mwenye Nguvu, Msamehevu.โ€ (35:28) Wataalamu (wanazuoni) kwa mnasaba wa aya hizi si wale waliobobea kwenye fani ya fiq-h tu na nyinginezo zinazoitwa za โ€œdiniโ€ bali ni pamoja na wale walio zama kwenye fani mbali mbali za elimu ya mazingira. Kwa mujibu wa aya hizi, wataalamu waliopigiwa mfano ni wale waliobobea katika taaluma ya hali ya hewa (meteorologists), katika taaluma ya madini (Geologists), katika taaluma ya matunda (horticulturist), katika taaluma ya wanyama (Zoologist) na katika taaluma ya watu na tabia zao (anthropologists). Wale ambao hawatumii vipawa vyao vya akili katika kumfahamu Mola wao kutokana na mazingira wamefananishwa na wanyama, kama tunavyojifunza katika Qur-an: โ€œNa bila shaka tumewaumbia moto wa Jahannam wengi katika majini na watu (kwa sababu hii) Nyoyo (akili) wanazo, lakini hawafahamu kwazo, macho wanayo lakini hawaoni kwayo na masikio wanayo lakini hawasikii kwayo Hao ni kama wanyama bali wao ni wapotofu zaidi. Hao ndio walioghafilika. (7:1 79) โ€œHakika vinyama viovu mbele ya Mwenyezi Mungu ni hawa wanaojipa uziwi na ububu ambao hawayatii akilini (wanayoambiwa au wanayoyaona)โ€ (8:22). Vilevile Alla(s.w) anawashutumu wale wanaobishana kuhusu Yeye pasina kuwa na elimu. Je! Huoni ya kw amba Mw enyezi Mungu amekutiishieni vilivyomo mbinguni na ardhini, na Akakukamilishieni neema zake zilizo dhahiri na za siri? Na wako watu wanaobishana katika (mambo) ya Mwenyezi Mungu pasipo elimu wala uwongofu wala Kitabu chenye nu ru (31:20) Na katika w atu w ako w anaojadiliana juu ya Mw enyezi Mungu bila ya ilimu wala uwongozi wala kitabu chenye nuru (22:8). Kutokana na aya hizi tunabainikiwa kwa uwazi kuwa katika Uislamu suala la kumuamini Allah (s.w) si suala la kibubusa (la kufuata mkumbo tu) bali ni suala la kitaaluma linalohitaji utafiti wa kina wa kisayansi. Kuna maeneo matano makubwa ambayo tukiyazamia vizuri kisayansi, yanatupatia dalili mbali mbali za uwazi zinazotuthibitishia kuwepo kwa Allah (s.w) na utukufu wake usio na mfano wake. Maeneo haya ni: Umbile la mbingu na ardhi na vyote vilivyomo ndani yake Nafsi ya mwanaadamu Historia ya mwanaadamu Maisha ya Mitume Mafundisho ya Mitume


                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1290

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Dalili za kuwepo mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtazamo wa uislamu juu ya Elimu, nini maana ya elimu na nani aliye elimika.

Ni nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika? Uislamu una mtazamo gani juu ya Elimu?

Soma Zaidi...
Athari za vita vya Uhud

Vita vya uhudi viliweza kuleta athari nyingi. Post hii itakuletea athari baadhi za vita hivyo.

Soma Zaidi...
ALAMA YA MUUMINI WA UKWELI KATIKA UISLAMU

ุนูŽู†ู’ ุฃูŽุจููŠ ู‡ูุฑูŽูŠู’ุฑูŽุฉูŽ ุฑูŽุถููŠูŽ ุงู„ู„ู‡ู ุนูŽู†ู’ู‡ู ุฃูŽู†ูŽู‘ ุฑูŽุณููˆู„ูŽ ุงู„ู„ูŽู‘ู‡ู ุตู„ู‰ ุงู„ู„ู‡ ุนู„ูŠู‡ ูˆ ุณู„ู… ู‚ูŽุงู„ูŽ: "ู…ูŽู†ู’ ูƒูŽุงู†ูŽ ูŠูุคู’ู…ูู†ู ุจูุงูŽู„ู„ูŽู‘ู‡ู ูˆูŽุงู„ู’ูŠูŽูˆู’ู…ู...

Soma Zaidi...
Tofauti kati ya Quran na vitabu vingine vya mwenyezi Mungu

Nguzo za imani (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Sifa za Wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Munaafiqun

Wanapokujia wanafiki, husema: "Tunashuhudia ya kuwa kwa yakini wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Soma Zaidi...
Kuamini mitume wa mwenyezi Mungu

Nguzo za Imani (EDK form 2:. Dhana ya elimu ya uislamu

Soma Zaidi...