1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)

1.

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W)

1.0 NJIA ZA KUMJUA MWENYEZI MUNGU (S.W).
Njia za Kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w).
a)Nafasi ya Fitrah (maumbile).
- Kila Mwanaadamu amepandikizwa hisia za kimaumbile zinazomtambua Mungu kupitia ujuzi wa kutambua mema na maovu.

- Mwanaadamu akipatwa na raha au misukosuko na huzuni hukiri uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (17:67), (30:30) na (91:7-8).



b)Vipaji vya Binaadamu.
- Vipaji vya akili na milango ya fahamu na fani zingine za elimu ni nyenzo pekee zikitumiwa vilivyo humuwezesha mtu kumjua Mola wake.
Rejea Qur’an (3:190-191), (35:28).



c)Nafsi ya mwanaadamu.
- Mfumo mzima wa mwili wa mwanaadamu na utendaji wake wa kazi wa ajabu wa viunge mbali mbali vya mwili kama kuyeyusha chakula tumboni, msukumo wa damu mwilini, n.k. ni ishara tosha juu ya uwepo wa Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (51:20-21)



d)Mazingira.
- Utegemezi na uhusiano wa kimahitaji ya kutumia rasilimali ya kuishi kati ya mimea, wanyama na binaadamu (ecological balance).

- Maumbile mengine kama mbingu, ardhi na yote yanayoonekana na yasiyooneka katika mazingira yanayotunguka.
Rejea Qur’an (3:190).



e)Wahyi (Ufunuo).
- Wahyi ndio nyenzo kuu ya kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mwenyezi Mungu (s.w) kwa usahihi unaotakikana.

- Elimu, vipaji na ujuzi au sayansi pekee haviwezi kumwezesha mwanaadamu kumtambua Mungu kwa baadhi ya maeneo, mfano nguzo za imani, n.k.



                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Main: Dini File: Download PDF Views 2570

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉4 Madrasa kiganjani    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana: