(f)Kujiepusha na kula mali ya YatimaWaumini wanawajibika kuwatunzia mayatima mali zao na kuwakabidhi wanapofikia baleghe yao baada ya kuwajaribu na kuthibitisha kuwa wanao uwezo wa kutunza mali zao - Rejea Qur-an (4:5-6).Katika aya ya (17:34) tunakatazwa hata kukurubia mali ya yatima kwa maana ya kwamba tusithubutu kuchanganya mali zao na zetu kwa kisingizio chochote kile na tusizitumie hata kwa matumizi yao wenyewe iwapo tunao uwezo wa kuwalea pasina kuhitajia mali zao:


"Na wapeni mayatima mali zao wala msibadilishe kibaya kwa kizuri. Wala msile mali zao pamoja na mali zenu. Hakika (yote) hayo ni jukumu kubwa." (4:2)“Na waogope (Mawasii kuwadhulumu mayatima; na wakumbuke) kama na wao wangewacha nyuma yao watoto madhaifu wangekuwa na khofu juu yao; basi wamwogope Mwenyezi Mungu na waseme maneno yaliyo sawa (kwa hao mayatima waliousiwa kuwatazama). Hakika wale ambao wanakula mali ya may atima kwa dhuluma, bila shaka wanakula moto matumboni mwao; na wataungua katika huo Moto (wa jahannam) uwakao.” (4:9-10)