Lengo la kuletwa mitume

Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukavitere..

Lengo la kuletwa mitume

Lengo la kuletwa Mitume wa Allah (s.w)


Mitume wameletwa kuwa Waalimu na viongozi wa kuwafundisha watu Uislamu na kuwaelekeza kuusimamisha Uislamu katika jamii kinadharia na kimatendo kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Kwa hakika Tuliwapeleka Mitume wetu kwa dalili wazi wazi na Tukaviteremsha vitabu na Uadilifu (mizani) pamoja nao, ili watu wasimamie uadilifu. (57:25)“Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na kw a dini ya haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa washirikina watachukia.” (9:33, 61:9)



Waumini wa kweli wa Mitume wa Allah (s.w) ni wale wenye tabia ifuatayo:


1. Kuwatii Mitume ipasavyo kwa kufanya yale yote waliyoamrisha na kuacha yale yote waliyoyakataza kama Qur’an inavyosisitiza:“... Na anachokupeni Mtume basi pokeeni, na anachokukatazeni jiepusheni nacho...” (59:7)Sem a: “Ikiw a nyinyi mnampenda Mw enyezi Mungu, basi nifuateni;(hapo)Mw enyezi Mungu atakupendeni na atakughufirieni madhambi yenu.Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghufira, mwenye rehema.Sema: “Mtiini Mwenyezi Mungu na Mtume. Na kama mkikengeuka, (Mw enyezi Mungu atakutieni adabu), kw ani Mw enyezi Mungu haw apendi Makafiri” (3 :31-32)



2.Kuwafanya Mitume vigezo vya maisha yao kibinafsi, kifamilia na kijamii kama inavyosisitizwa katika Qur-an:“Bila shaka mnao mfano mwema (wa kuiga) kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, kwa mwenye kumuogopa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho, na kumtaja Mwenyezi Mungu sana ”. (33:21)



3.Kuwapenda Mitume kuliko nafsi zao kama Qur-an inavyosistiza:“Sema “Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali m lizozichum a na biashara mnazoogopa kuharibikiw a,na majumba mnayoyapenda; (ikiwa vitu hivi) ni vipenzi zaidi kw enu kuliko Mw enyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mw enyezi Mungu alete am ri yake; na Mw enyezi Mungu hawaongozi watu maasi” (9:24)
Kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume si jambo lingine zaidi ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa unyenyekevu na upendo. Muumini wa kweli hatakuwa tayari kuifurahisha nafsi yake au kumfurahisha yeyote awaye kinyume na kumfurahisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ni katika maana hii Mtume (s.a.w) anasema:
“Hatakuwa mmoja wenu ni Muumini wa kweli mpaka anipende zaidi kuliko chochote kile ikiwa ni pamoja na familia yake, mali yake na watu wote”.(Sahihi Muslim)
“Yeyote yule anayependa Sunnah yangu ananipenda, na yeyote yule anayenipenda atajikuta yuko ubavuni kw angu huko Peponi.” (Tirm idh)



4. Kuwafanya Mitume kuwa Mahakimu wao pale wanapohitilafiana katika jambo lolote lile kama tunavyojifunza katika Qur-an:“Naapa kwa (haki ya) Mola wako (Ewe Muhammad); wao hawawi wenye kuamini mpaka wakufanye hakimu katika yale wanayokhitalifiana, kisha wasione uzito nyoyoni mwao juu ya hukumu uliyopitisha, na wanyenyekee kabisa.” (4:65)“Haiwi kwa mwanamume aliyeamini wala kwa mwanamke aliyeamini, Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri, wawe na hiyari katika shauri lao. Na mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu (upotevu) ulio wazi. ” (33:3 6)



5.Kuwa na yakini kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) ndiye Mtume wa mwisho kama Qur-an inavyosisitiza:“Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali yeye ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na mwisho wa Mitume, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila kitu.” (33:40)



6.Kumswalia Mtume(s.a.w) mara kwa mara katika swala na kila anapotajwa. Kumswalia Mtume(s.a.w) ni amri ya Allah(s.w) kama inavyotuelekeza ifuatavyo:Hakika Mwenyezi Mungu anamteremshia Rehema Mtume;na Malaika wake. Basi; Enyi mlioamini,




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Tawhid Main: Dini File: Download PDF Views 1736

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Makemeo juu ya Zinaa na Hukumu kwa Wazinifu.

Tendo la zinaa ni tendo chafu kimaadili na Allah (s.

Soma Zaidi...
Muumini ni yule ambaye anazungumza ukweli

Ukweli ni katika sifa za waumini. Siku zote hakuna hasara katika kusema ukweli. Kinyume chake uongo ni katika madhambi makubwa sana.

Soma Zaidi...
Lengo la ibada maalumu

Lengo la ibada maalumu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa

Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao

Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s.

Soma Zaidi...
Kwanini mwanadamu hawezi kuishi bila ya dini?

Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...