Maswali juu ya dini anayostahiki kufuata mwanadamu
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Zoezi la 1.
- (a) Nini maana ya Dini.
(b) Dini sahihi ni lazima imfikishe mwanaadamu katika kufikia lengo la kuumbwa kwake. Ainisha sifa za dini sahihi inayostahiki kufuatwa na mwanaadamu.
- Mwanaadamu pamoja na ujuzi alionao, hawezi kujiundia mfumo (dini) sahihi wa maisha. Thibitisha kauli hii kwa hoja tano tu.
- (a) Bainisha nyezo kuu anazozitumia mwanaadamu katika kujielimisha na madhifu yake.
(b) Nini maana ya kusimamisha Uislamu katika jamii?
- Mwanaadamu pamoja na kudai kutofuata dini yeyote, bado hawezi kuepukana nayo. Eleza ni kwanini dini kwa mwanaadamu ni jambo lisilobudi.
- Jihad ni jambo la muhimu katika kuupatia Uislamu heshima yake ndani ya jamii. Thibitisha umuhimu wa jihad katika kuusimamisha Uislamu.
- Ainisha matunda yatakayopatikana kwa Uislamu kusimama na kuongoza maisha ya jamii.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 kitabu cha Simulizi π2 web hosting π3 Dua za Mitume na Manabii π4 Simulizi za Hadithi Audio π5 Kitabu cha Afya π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Kutowatii Wazazi katika kumuasi Allah (s.w)
"Na (wazazi wako) wakikushurutisha kunishirikisha na (yale) ambayo huna ilimu nayo, usiwatii; lakini kaa nao kwa wema hapa duniani (Maadamu ni wazee wako, ila usiwafuate tu mwenendo wao mbaya); Shika mwenendo wa wale wanaoelekea kwangu, kisha marejeo yenu
Soma Zaidi...Himizo la kuwasamehe waliotukosea
βNa wasiape wale wakarimu na wenye wasaa miongoni mwenu, kujizuia kuwasaidia jamaa zao, maskini na wale waliohama kwa ajili ya Dini ya Allah; na wasamehe na waachilie mbali (wapuuze yaliyopita).
Soma Zaidi...