Lengo la kuumbwa Mwanadamu ni lipi?


image


Kwenye kipengele hichi tutajifunza lengo la kuumbwa mwaanadamuengo la kuumbwa ulimwengu na viumbe vilivyomo.


5.2 .Lengo la Kuumbwa mwaanadamu.

  • Lengo la kuumbwa Mwanaadamu.

-     Ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) katika kila kipengele cha maisha ya kila siku ya kibinafsi, kifamilia na kijamii.

      “Sikuwaumba Majini na Binaadamu ila wapate kuniabudu” (51:56).

 

-     Mwanaadamu yeyote anayetambua lengo hili, na kuishi kwa mujibu wa lengo ndiye mwenye akili.

      Rejea Qur’an (3:190-191).

 

-     Kunasibisha ibada maalumu kama ndio lengo kuu la kuumbwa mwanaadamu sio sahihi kwani kila ibada maalumu ina lengo lake maalumu na pia utekelezaji wake ni sehemu ndogo sana katika kumuabudu Allah (s.w).

 

-     Kwa mfano; shahada ina 0%, swala 7% , zaka 2½%, swaum 5% na hija 0% ikiwa ni jumla ya 3% ya utekelezaji wa nguzo zote 5 za Uislamu ndio ziko katika ibada na 97% ni nje ya ibada.

 

-     Hivyo, lengo la kuumbwa mwanaadamu litafikiwa tu kwa kufanya ibada masaa 24 katika kila kipengele cha maisha na sio baadhi ya vitendo fulani tu.

      Rejea Qur’an (2:208), (3:102).

 

 

  • Lengo la kuumbwa Ulimwengu na viumbe vilivyomo.

-     Ni kumtumikia mwanaadamu ili kufikia lengo la kuumbwa kwake kwa kuboresha maisha yake.

 

-     Maumbile na viumbe vyote vinavyomzunguka mwanaadamu vimetiishwa kwake ili aweze kuvitumia katika kutekeleza ibada.

      Rejea Qur’an (45:13).

 

-     Akili, elimu, fani, ujuzi na vipawa vya mwanaadamu ndio nyenzo zitakazomuwezesha kuyamiki na kuyamudu mazingira yake na kuendesha ibada ipasavyo.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Download App zetu hapa ujifunze zaidi       ðŸ‘‰    2 Jifunze Fiqh       ðŸ‘‰    3 Madrasa kiganjani offline       ðŸ‘‰    4 Tunakukaribisha kwenye Maktaba yetu    


Je una maswali, maoni ama ushauri, tutumie sms ✉ bofya hapa hapa, ama wasiliana nasi kwa WhatsApp bofya hapa



Post Nyingine


image Haki za viumbe na mazingira
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Mafunzo yatokanayo na upinzani wa maquraish dhidi ya uislamu
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Kujiepusha na ria na masimbulizi
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Madhumuni ya dola ya uislamu
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Nguzo za imani
Zifuatazo Ni nguzo za imani (EDK form 2: elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Funga za Sunnah na namna ya kuzitekeleza
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Wanaostahiki kupewa sadaqat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...

image Mafunzo yatokanayo na kuanzishwa kwa dola ya uislamu madinah
Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

image Uandishi wa hadithi wakati wa tabiina (wafuasi wa maswahaba)
Sunnah na hadithi (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...