Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo: (i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu.
Ushahidi wa kuthibitisha kutendeka kwa kosa la uzinifu unapatikana kwa namna tatu zifuatzo:
(i)Kushuhudia tendo hilo likifanyika kwa wakati mmoja watu wanne Mukalafu (Walio baleghe na wenye akili timamu), wakiwa ni Waislamu waadilifu.
(ii)Muhusika au wahusika kukiri kwa hiari yake/yao bila ya shinikizo au mazingira yanayopelekea shinikizo lolote.
(iii)Mwanamke kupata ujauzito nje ya ndoa.
Nje ya ushahidi huu, mtu hatahukumiwa kwa kosa la uzinifu au ubasha pamoja na kuwepo mazingira ya kutatanisha. Sana sana atahukimiwa kukurubia zinaa na kupewa nasaha na maonyo stahiki. Ila ikitokea kwa mwanandoa kumkamata mwenziwe ugoni, bila ya mashahidi wanne au muhusika kukiri kosa kwa hiari yake, wanandoa hawa watalazimika kula kiapo mbele ya kadhi kama ilivyoelekezwa katika aya zifuatazo:
Na wale wanaowasingizia wake zao (kuwa wamezini) na hawana mashahidi ila nafsi zao, basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudilia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu: ya kwamba bila shaka yeye ni mmoja wa wanaosema kweli. Na mara ya tano (aape) kwamba laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.Na (mke) itamuondokea adhabu kwa kutoa shahada mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu ya kwamba (huyu mume) ni miongoni mwa waongo.
Na mara ya tano (aape) ya kwamba hasira ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake kama (mumewe) yu miongoni mwa wanaosema kweli, (na yeye mke ndiye muongo)." (24:6-9)
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Yale tunayoamrishwa kushikamana nayo ni haya yafuatayo: (i)Kumuabudu Allah (s.
Soma Zaidi...Kuamini Malaika ni imani ambayo pindi ikithibiti vema moyoni, huleta taathira kubwa sana katika maisha ya kila siku na hivyo kubadili kabisa tabia na mwenendo wa Muumini.
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mtazamo wa uislamu juu ya dini (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Bila shaka wanaume wenye kufuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanawake wanaozifuata vizuri nguzo za Uislamu, na wanaume wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanawake wanaoamini vizuri nguzo za Imani, na wanaume wanaotii, na wanawake wanaotii, na wanaume wa
Soma Zaidi...