Pia sifa za Waumini zinabainishwa katika Suratul-Muuminuun katika aya zifuatazo:
Hakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao huwa wanyenyekevu. (23:1-2)
Na ambao hujiepusha na Lagh-wi (mambo ya upuuzi). Na ambao (nguzo ya) Zaka wanaitekeleza. (23:3-4)
Na ambao tupu zao wanazihifadhi isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale iliyomiliki mikono yao ya kuume. Basi hao ndio wasiolaumiwa. (23:5-6)
Lakini anayetaka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka. Na ambao amana zao na ahadi zao wanaziangalia. (23: 7-8).
Na ambao swala zao wanazihifadhi. Hao ndio warithi. (23:9-10)
Ambao watarithi Firdaus (Pepo ya daraja ya juu wakae humo milele. (23:11)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa, waumini wa kweli waliofuzu na watakaostahiki kupata Pepo ya Firdaus, (ya daraja ya juu kabisa) ni wale wanaojipamba na sifa zifuatazo:
(i)Wenye Khushui katika Swala
Waumini wa kweli waliofuzu huwa na khushui (unyenyekevu) katika swala. Yaani huswali kwa kutulizana kimwili, kimoyo na kifikra, huku wakizingatia yale wayasemayo mbele ya Mola wao wakiwa na yakini kuwa anawaona na anawasikia.
(ii)Wenye Kuhifadhi Swala
Waumini wa kweli waliofuzu huhifadhi swala kwa kutekeleza kwa ukamilifu sharti zote za swala, nguzo zote za swala na huswali kama alivyoswali Mtume (s.a.w) na hudumu na swala katika maisha yao yote. (Qur-an 70:23)
Zingatio:
Swala husimama kwa kuhifadhiwa na kuswaliwa kwa khushui na kudumu na swala katika maisha yote.
(iii) Wenye kuepuka Lagh-wi
Waumini wa kweli waliofuzu hujiepusha na Lagh-wi. Laghwi ni mambo ya upuuzi yanayomsahaulisha mtu kumkumbuka Mola wake, yanayosababisha ugomvi au bughudha baina ya watu na yanayomsahaulisha mtu kuswali (Qur-an 5:91). Mahala ambapo Allah (s.w) hakumbukwi, shetani huchukua nafasi. michezo yote ni lagh-wi isipokuwa ile tu inayochezwa kwa kuchunga mipaka yote ya Allah (s.w) kwa lengo la kukuza ukakamavu na siha ili kuwa imara katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
(iv)Hutoa Zakat na Sadakat
Waumini wa kweli waliofuzu hutoa Zakati wakiwa na mali na hutoa misaada na huduma waziwezazo kwa wanaadamu wenziwe kwa kadiri ya haja ilivyojitokeza. Asiyejali binaadamu wenzake, huku ana uwezo si Muumini. Rejea Qur-an (107:1-3).
(v)Wenye kujiepusha na Zinaa na Tabia za Kizinifu.
Waumini wa kweli waliofuzu hujihifadhi na zinaa au hujiepusha kufanya jimai nje ya mipaka aliyoiweka Allah (s.w). Hatua ya kwanza ya kujilinda na zinaa ni kujiepusha na vishawishi vyote vinavyokurubisha watu kwenye zinaa. Muumini wa kweli hutekeleza pasina kusita ile amri ya Allah (s.w) ya katazo kuwa:
Wala usiikaribie zinaa; kwa hakika huo ni uchafu na ni njia mbaya kabisa. (17:32)
(vi)Huwa Muaminifu
Waumini wa kweli waliofuzu huchunga amana. Hutunza amana aliyopewa na kuirejesha au kuitumia kwa mujibu wa maelekezo ya mwenyewe. Amana kuu aliyopewa mwanaadamu na Mola wake ni kule kufadhilishwa kwake kuliko viumbe vingine vyote (Qur-an (17:70),(95:4) ili asimamishe Ukhalifa (utawala wa Allah) katika ardhi kama tunavyokumbushwa katika Qur-an:
"Kwa yakini Sisi tulidhihirisha amana kwa mbingu, ardhi na milima, vikakataa kuichukua na vikaiogopa, lakini mwanaadamu aliichukua. Bila shaka yeye ni dhalimu mkubwa, mjinga sana." (33:72)
(vii)Wenye Kutekeleza Ahadi
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.w). Ahadi kubwa wanayotoa Waislamu mbele ya Allah (s.w) ni Shahada; pale wanapoahidi kuwa hawatamshirikisha Allah (s.w) na chochote na kwamba wataishi maisha yao yote kwa kufuata mwongozo wa Allah (s.w) kupitia kwa Mtume wake, Muhammad (s.a.w).
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 587
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Simulizi za Hadithi Audio
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Kitabu cha Afya
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Uchambuzi wa Neema Alizopewa Nabii Sulaiman(a.s)
(i) Kutiishiwa Upepo Qur'an inatufahamisha kuwa Nabii Sulaiman alitiishiwa upepo akaweza kuutumia apendavyo kwa amri yake. Soma Zaidi...
Dalili Kubwa za kukaribia Siku ya kiama
Soma Zaidi...
Maana ya Elimu katika uislamu na nani aliye elimika?
Hili ni swali kutoka katika maarifa ya elimu ya dini ya kiislamu kidato cha kwanza (EDK FORM 1) Soma Zaidi...
Imani ya Kiislamu na ni nani muumini?
Soma Zaidi...
ENYI WAJA WANGU NIMEIKATAZA NAFSI YANGU DHULMA
Soma Zaidi...
Kwa namna gani nabii Musa na Bi Mariam waliweza kuzungumza na Allah nyuma ya pazia
Nabii Musa na Mama yake nabii Isa bi Mariam waliweza kuwasiliana na Allah nyuma ya pazia. Soma Zaidi...
Kuangamizwa Waovu na Kuokolewa Waumini
Baada ya kuonywa wasionyeke, Allah(s. Soma Zaidi...
Mambo muhimu anayofanyiwa muislamu kabla ya kufa
Dhana ya faradh kwa muislamu (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Kwanini Uislamu Ndio Dini Pekee Inayostahiki Kufuatwa na Watu?
Soma Zaidi...
Nafsi ya mwanaadamu
Soma Zaidi...
Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Soma Zaidi...